Umoja wa Mataifa wataka hatua kuchukuliwa dhidi ya tabia ya wanawake kufungwa kizazi kwa lazima


Zishilo Dludla looking out of a window

Chanzo cha picha, BBC News

Maelezo ya picha,

Ushahidi wa kulazimishwa kufungwa kizazi umepatikana katika nchi 38 miaka 20 iliyopita.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ieonesha kuwa takriban nchi 38 zimeendeleza tabia ya kufunga kizazi kwa lazima katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, huku baadhi ya kesi hizo zikijumuisha wanawake waliofungwa kizazi kinyume na matakwa yao wakati wanajifungua.

Umoja wa Mataifa imetoa wito wa kusitishwa kwa tabia ya kufunga watu kizazi kinyume na matakwa yao ambayo imejitokeza katika kila bara duniani kulingana na utafiti uliofanywa na Profesa Sam Rowlands, na kutaka serikali ichukue hatua dhidi ya wanaotekeleza tabia hiyo.

Jamii za waliowachache, wanawake wanaoishi na ugonjwa wa virusi vya HIV na makundi ya waliotengwa ikiwemo waliobadilisha jinsia zao wote wamejikuta katika hali kama hizo kote duniani.

“Kuna historia ndefu ya ubaguzi duniani na nyanyasaji unaohusishwa na kufungwa kizazi kwa lazima, ambayo bado inaendelea hadi hii leo,” anaelezea Dr. Tlaleng Mofokeng, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki ya kupata afya. “Hilo pekee, ni ukukaji mkubwa wa haki za binadamu.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *