Unayopaswa kujua juu ya azma ya wapinzani ya kumshitaki Trump


Donald Trump in the Oval Office, February 2017

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Wapinzani wa Democrats wanasema Ikulu ya White house ya Trump imefikia katika kile walichokiita “kiwango cha kabuli jipya lisilokuwa na sheria”

Si jambo la kawaida unashuhudia rais akiwa katika hatari ya kutimuliwa madarakani na bunge.

Kwa hiyo kama wewe ni mpenzi wa masuala ya siasa, basi usipitwe na maigizo makubwa wakati bunge la Congeress litakapoanza kusikiliza uchunguzi rasmi dhidi ya Trump mbele ya umma kuanzia tarehe 13.

Unaweza pia kusoma:

Uchunguzi huu una maana gani?

Uchunguzi huu ni aina ya mahojiano ya kesi ambayo yanaweza kupelekea kung’olewa madarakani kwa rais na bunge la Kongresi.

Baadhi ya watu wanafikiria kuwa uchunguzi huu ni hatua halisi ya kumg’oa madarakani rais wa nchi , lakini ukweli ni kwamba ni mwanzo tu wa mchakato wa hatua mbili ambazo hufanyika katika mabunge mawili ya Marekani.

Haki miliki ya picha
Empics

Image caption

Bunge dogo huamua ikiwa rais atashtakiwa katika seneti

Kwanza wabunghe katika Baraza la wawakilishi huangalia ushahidi na kuamua ikiwa wanataka kushinikiza mashtaka dhidi ya rais – au kama kama inavyoelezwa ”kupendekeza kufanyiwa uchunguzi wa tuhuma “.

Lakini ni bunge la juu zaidi, ama Seneti, lenye mamlaka ya kuendesha kesi, ikiwa rais atapatikana na hatia, halafu yeye anaondolewa mamlakani makamu wa rais huapishwa.

Ni marasi wangapi wa Marekani ambao wamewahi kushtakiwa?

Ni wawili tu: Andrew Johnson mwaka 1868 na Bill Clinton mwaka 1998. Wote walichunguzwa katika bunge lakini baadaye Seneti ikawaondolea hatia.

Mnamo mwaka 1974, rais Richard Nixon alipatkana akiwa anawafanyia ujasusi wapinani wake katika sakata inayofahamika kama Watergate – alijiuzulu kwasababu alijua kuwa atahojiwa mbele ya bunge na kung’olewa madarakani na Senati

Vipi kuhusu Trump– ni kwanini anakabiliwa na uchunguzi huu?

Donald Trump anashutumiwa kutumia vibaya mamlaka aliyonayo na kufanya mchezo mchafu ili kuongeza nafasi yake ya kuchaguliwa tena mwaka ujao.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Trump anashutumiwa kuacha kutoa usaidizi wa kijeshi kwa Ukraine ili kuilazimisha nchi hiyo imchunguze hasimu wake kisiasa

Anadaiwa kumshinikiza rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, kuchunguza taarifa zinazoichafulia jina familia ya Joe Biden – aliyekuwa Makamu wa rais wa Barack Obama ambaye naaminiwa kuwa anaweza kuwa mshindani mkuu wa Trump katika kinyang’anyiro cha kuingia ikulu ya White House 2020.

Je Trump alivunja sheria?

Si kila mtu anakubali kwamba lazima uchunguzwe kwa njia hii eti kwa sababu tu ulimuomba kiongozi wa taifa la kigeni kusaka taarifa chafu juu ya hasimu wako.

Trump anasema hakufanya kosa lolote na ameuita uchunguzi huu dhidi yake mchakato wa “dhaifu, udanganyifu, wa kuvuruga mambo na wenye upendele wa hali ya juu ” . Ikulu ya White House inasema kuwa haitafanya ushirikiano wowote katika uchunguzi huu.

Lakini amekuwa katika kipindi kigumu tangu mfichuaji wa sakata hii alipolalamika juu ya simu aliyompigia rais wa Ukraine Zelensky tarehe 25 Julai.

Trump alikuwa amezuwia mamilioni ya dola ya msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine na maafisa wa ngazi ya juu wamesema kuwa alilweka wazi kwamba hatatoa pesa hadi pale Ukraine itakapoanza uchunguzi dhidi ya hasimu wake. Ikulu ya Marekani inakanusha hili.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Spika Nancy Pelosi aliziambia kamati sita kuendelea na uchunguzi chini ya mwavuli wa uchunguzi dhidi ya Trump

Na ni nini kitakachofuata ?

Uchunguzi utafanywa na wabunge katika makundi madogo madogo, yanayoitwa kamati. Kila kamati litabobea katika masuala ambayo yatakuwa ni ya muhimu kwa kesi, kwa mfano , masuala ya kigeni, matumizi ya fedha na sheria. Pia watawaleta mashahidi kutoa ushahidi mbele ya umma.

Mawakil wa rais wataruhusiwa kushiriki

Kama kamati itaamua kupendekeza mashtaka dhidi ya rais , basi Bunge la wawakilishi litapiga kura.

Unaweza pia kusoma:

Kuna uwezekano upi wa mashtaka?

Ni wabunge wachache tu wanaotakiwa katika hatua hii kumshitaki rais . Kwa kuwa chama cha upinzani cha Democratic kina wingi wa viti bungeni, kuna uwezekano mkubwa kwamba Trump atashtakiwa.

Maafisa wakuu wa Democratswamekwisha kusema kwamba wanataka kura hii kupigwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Andrew Johnson ( Kushoto) na Bill Clinton ( Kulia) walishtakiwa katika bunge na kuondolewa mashtaka na bunge la Seneti, huku Nixon (katikati) akijiuzulu baada ya kukaribia kuondoshwa mamlakani

Na kuna uwezekano wa kiasi gani kwamba Trump ataondoka mamlakani?

Hajafunga vilago vyake bado. Chama chake cha Republican kina udhibiti kikiwa na viti 53 kati ya 100 katika Seneti na theluthi mbili ya kura zinahitajika kumuondoa kabisa rais kazini.

Kwa hiyo labda idadi kubwa – takiban wabunge 20 wa chama chake wamgeuke , Trump bado ataendelea kubaki pale alipo. Kwa sasa wanachama wa Republican bado wanamuunga mkono.

Je uchunguzi huu sasa una maana gani je ni maigizo tu ya kisiasa?

Wafuasi wa Trump swanaamini kuwa upinzani unajaribu kumaliza nguvu wapiga kura wa rais. Mchakato huu unaweza kuharibu sura ya rais.

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Matokeo ya uchunguzi huu kwa vyovyote yatakuwa na athari katka uchaguzi wa 2020

Lakini unaweza kuamini maneno ya Spika wa bunge MDemocratic , Nancy Pelosy, ambaye anafikiri Ikulu ya White House ya Trump inaongozwa kama ” kaburi jipya lisilo na sheria”.

Wapinzani wa rais wa Marekani Donald Trump wanataka kufungua kesi dhidi yake juu ya matumizi mabaya ya mamlaka . Ikiwa watafanikiwa, atakabiliwa na mchakato wa mchakato wa kuhojiwa na bunge- jambo ambalo liliwahi kufanyika dhidi ya marais wawili tu wa Marekani kabla yake – na anaweza kuondoshwa mamlakani. Huku joto la kisiasa likipanda mjini Washinington , haya ndiyo unayopaswa kufahamu kuhusu sakata hili

Bilionea aliyegeuka na kuwa mwanasiasa amekuwa katika utata kadhaa wa kisheria , mkiwemo uchunguzi juu ya matai ya uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 , hatua yake ya kukataa kufichua nyaraka juu ya kodi na madai ya malipo kwa mwanamke ambaye anasemekana alikuwa na mahusiano nae.

Suala la Ukraine na Biden linaweza kuwa ni la mwisho katika orodha ya ukiukaji wa maadili.

Lakini kumbuka uchunguzi pia ni hatari sna kwa upinzani – Kama uchunguzi hautafika popote, unaweza kuwaathithi katika uchaguzi wa 2020, kuwaumiza Democrats katika maeneo yenye ushindani mkubwa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *