Uvamizi wa nzige: Umoja wa Mataifa waonya njaa katika Ethiopia, Kenya, Uganda, Tanzania na Somalia


Nzige

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Kuna hofu ya mabilioni ya nzige-ambazo zinaweza kuongezeka

Kanda ya Afrika Mashariki inaweza kukumbwa na njaa kama wimbi la nzige wanaokula mimea kwa haraka na malisho ya mifugo hawatadhibitiwa, afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC.

Itasababisha mzozo wa chakula, Dominique Burgeon, mkurugenzi wa shughuli za dharura wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa(FAO), amesema.

Ethiopia, Somalia, Kenya, Tanzania na Uganda zimeathiriwa na nzige.

Juhudi za kudhibiti wadudu hao hadi sasa hazijafanikiwa .

Unyunyiziaji wa dawa ya kuua wadudu ndio njia bora zaidi ya kukabiliana na nzige lakini nchi katika kanda hiyo hazina raslimali zinazofaa kukabiliana nao.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *