Uvumbuzi wa pembe bandia za faru kupambana na soko haramu la pembe za faru


Faru

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Wanyama aina ya faru wako hatarini kupotea

Wanasayansi wabuni njia ya kutengeneza pembe bandia ya faru, ambayo wana matumaini kuwa italidhoofisha soko la magendo .

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Oxford na Fudan cha China wamepata njia ya kutengeneza pembe bandia kwa gharama nafuu kutokana na manyoya ya Farasi.

Uhitaji wa pembe za faru umekuwa ukichochea kwa kiasi kikubwa shughuli zaujangili na kutishia maisha ya viumbe hao.

Timu ya Oxford imesema utengenezaji wa pembe bandia ”utaivuruga biashara hiyo haramu”.

Lakini kumekuwa na maoni tofauti kuhusu kama njia hii inaweza ikawa na mafanikio.

Taasisi ya kutetea haki za faru ya Save the Rhino International imesema ni muhimu kulenga hatua za kupambana na ujangili na kujaribu kupunguza uhitaji wa wateja.

Mradi utafanikiwa vipi?

Pembe za faru zinadaiwa kuhitajika kwenye sekta ya dawa asilia nchini China- sekta ambayo imeendelea kusukuma biashara hii ingawa mamlaka zimekuwa zikipiga marufuku biashara hii.

Mradi huu wa Uingereza na China ni jaribio jipya kutafuta njia ya kutengeneza pembe bandia ionekane kama ya kweli na yenye kushawishi, ikiwa na lengo la kujaza soko hilo kwa pembe za faru zilizo bandia na kushusha gharama za malipo ya majangili na wasafirishaji wa nyara hizo.

Awali kulijitokeza mawazo ya kuwa na pembe bandia, lakini mradi huu unataka aina ya pembe ambazo zitazalishwa kwa wingi na kwa gharama nafuu.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Utengenezaji wa pembe bandia unalenga kukomesha biashara ya pembe duniani

Wanasayansi wanasema ”pembe” za faru si kama pembe za Ng’ombe, lakini zinaundwa kwa manyoya ya farasi yaliyowekwa gundi pamoja.

Na timu ya wanasayansi wa wanyama chuoni Oxford na walio chuo cha Fudan mjini Shanghai wamebuni njia ya kutengeneza manyoya ya farasi na kuwa na muonekano wa kuutazama na kugusa mithili ya pembe halisia, hata kama pembe hiyo ya bandia ilikatwa.

Ikiwa pembe za aina hiyo zitazalishwa kwa gharama ndogo, wanasayansi wanasema itaondoa gharama na malipo yatokanayo na mauaji ya faru.

Profesa Prof Fritz Vollrath kutoka Chuo cha Oxford amesema ana matumaini mbinu hii itatumika ”kuivuruga biashara na kuunga mkono jitihada ya kuwalida faru”.

Hofu ipo kuhusu madhara hasi ya mradi huu?

Lakini Mkurugenzi msaidizi wa shirika la Save the Rhino International, hashawishiki na kwa kiasi gani pembe bandia zitapunguza tishio dhidi ya faru.

Anasema kuwa kuna hatari kuwa jaribio la ”kujaza soko na pembe bandia” kutasababishwa madhara ambayo hayajakusudiwa ya kutanuka kwa soko na kusababisha ongezeko la uhitaji, ambao utasababisha ujangili uongezeke wa pembe halisi za faru.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *