Uzinduzi wa reli mpya ya SGR 'isioelekea kokote' wahojiwa Kenya


Uzinmduzi rasmi wa

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua rasmi awamu ya pili ya mradi wa reli wa mabilioni ya dola.

Kuna hofu huenda uzinduzi huo ukawa ikawa mwisho wa mradi huo mkubwa zaidi baada ya China kukataa kuufadhili.

Awamu ya pili ya ujenzi wa reli hiyo ilitarajiwa kuendelezwa hadi mpaka wa Kenya na Uganda (malaba).

Wataalamu wanautaja kuwa usafiri usioelekea kokote lakini Serikali inashikilia kuwa mradi huo mpya utakuwa na manufaa kwa makubwa.

Tofauti na uzindizi wa reli ya kutoka Mombasa hadi Nairobi, ilivvyozinduliwa kwa mbwembwe mwaka 2017, uzinduzi wa reli hii mpya haujapewa umuhimu mkubwa.

Wachambuzi wanasema Serikali inakabiliwa na wakati mgumu kuelezea faida za kiuchumi za mradi huo kwasababu baadhi ya vituo havuiina shughuli nyingi katika mkoa wa bonde la ufa.

Mpango wa kuendeleza ujenzi wa reli hiyo hadi Kisumu, kupitia ziwa Victoria, hadi Uganda umekatizwa na hatua ya China kujiondoa katika ufadhili wake.

Katika kongamano la viongozi wa bara la Afrika na China mjini mataifa ya Afrika mjini Beijing, Serikali ya ilisema itafadhi miradi iliyo na manufaa ya kiuchumi pekee.

Ujenzi wareli hiyo uligharimu dola bilioni 1.5 sawa na (euro bilioni 1.1).

Huduma ya wateja inatarajiwa kuanza wakati wowote huku ile ya mizigo ikifuatia baadae japo haija bainika inaanza lini

Uzindiliwa wa reli kati Mombasa-Nairobi pia ulizua suala la faida yake kiuchumi kwa taifa la Kenya.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *