Virusi vipya vya Corona: England yapiga marufuku safari za ndege kutoka mataifa sita ya Afrika


Maafisa wa afya wakipima virusi vya corona

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha,

Maafisa wa afya wakipima virusi vya corona

Wasafiri wanaowasili nchini England kutoka mataifa tofauti ya Afrika watalazimika kujitenga huku kukiwa na onyo kuhusu aina mpya ya virusi vya corona.

Waziri wa afya nchini Uingereza Sajid Javid alisema siku ya Ijumaa kwamba mataifa sita yataongezwa katika orodha , huku baadhi ya ndege zikipigwa marufuku kwa muda.

Mtaalamu mmoja alitaja virusi hivyo vipya kwa jina B1.1.529, kuwa hatari zaidi kuonekana kufikia sasa na kuna wasiwasi kwamba vina uwezo wa kukwepa kinga.

Hakuna hata kisa kimoja cha virusi hivyo kimeripotiwa nchini Uingereza. Ni wagonjwa 59 pekee waliogunduliwa nchini Afrika Kusini , Hong Kong na Botswana kufikia sasa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *