Virusi vya corona: EU kuruhusu wageni kutoka mataifa 14 'salama' kutembea


Passport control at Larnaca airport, Cyprus, file pic

Maelezo ya picha,

Udhibiti wa paspoti katika uwanja wa ndege wa Larnaca, Cyprus

Umoja wa ulaya (EU) umetaja majina ya nchi 14 ambazo wananchi wake wanadaiwa kuwa salama kuruhusiwa kuingia katika nchi zake kuanziA Julai, mosi , licha ya mlipuko uliopo lakini Marekani, Brazil na China hazipo katika orodha hiyo.

Mataifa yaliyotajwa ni pamoja na Australia, Canada, Japan, Morocco na South Korea.

Umoja wa ulaya ipo tayari kuiongeza China katika orodha kama tu serikali yake China itatoa ruhusa sawa kwa wasafiri wa umoja wa ulaya, mwanadiplomasia anasema.

Makatazo katika mipaka ya Umoja wa ulaya imeondolewa kwa wasafiri ambao ni raia wa Umoja wa ulaya kusafiri ndani ya ukanda wao.

Sheria zilizowekwa dhidi ya wasafiri wa Uingereza ziko tofauti na makubaliano ya Brexit.

Wananchi wa Uingereza wanachukuliwa sawa na raia wa Muungano wa Ulaya mpaka mwisho wa kipindi cha mpito Desemba, 31.

Katika orodha ya sasa, maeneo salama ambayo yanaweza kuongezwa ni Algeria, Australia, Canada, Georgia, Japan, Montenegro, Morocco, New Zealand, Rwanda, Serbia, South Korea, Thailand, Tunisia na Uruguay.

Kwa sasa Uingereza inafanya majadiliano na mataifa kadhaa ambayo ni wanachama wa Umoja wa ulaya, kuona namna ambavyo virusi vya corona kutozuia kabisa mapumziko ya wakati wa msimu wa watalii unaowaajiri mamilioni ya watu.

Jumanne majira ya mchana, Umoja wa Ulaya itarasimisha nchi gani inapaswa kuhukumiwa kuwa salama au hapana .

Mataifa mengi ya umoja wa ulaya – yapata 55% ya mataifa ya Umoja wa mataifa, ambayo inawasilisha 65% ya idadi ya watu wa Umoja wa ulaya ambao wako kwenye orodha.

Kuna mgawanyiko kati yao kama vile Spain – inataka kukuza utalii lakini inataka kujionyesha salama licha ya ugonjwa wa corona kuathiri nchi hiyo kwa ukubwa na nchi nyingine ni Ugiriki,na Ureno, ambazo zote zinategemea utalii lakini wanaogopa virusi.

Unaweza pia kusoma:

Unaweza kudhani kuwa itakuwa sawa moja kwa moja, kuamua mataifa gani ambayo hayapo kwenye umoja wa ulaya kutambuliwa kuwa salama.

Lakini inaonekana kuwa mchakato ambao hautakuwa na haki , unaweza kusababisha migogoro , kuchanganya masuala ya kisiasa na uchumi pamoja na afya ya umma.

Mataifa kama Ujerumani na Uhispania, wameathirika pakubwa na Covid-19,na zinataka kuonekana salama.

Wanataka kuwepo kwa orodha fupi ya mataifa ambayo yana maambukizi kwa kiwango kidogo, afya nzuri na data za uhakika za afya.

Ingawa Ugiriki na Ureno walikuwa na mawazo mengine.

Wana hofu ya kuongeza muda wa marufuku ya kutotoka nje, kuanguka kwa uchumi wake wa utalii na hawana hofu sana ya kuenea kwa maambukizi ya mlipuko, ilimradi tu wawepo kwenye orodha.

Na ukija upande wa Ufaransa, ambako wanasisitiza biashara katika mji wake.

Kama mataifa ambayo sio nchi wanachama wa Umoja wa ulaya wanazuiwa kuingia katika ukanda huo basi inabidi wasionekane katika orodha, Paris ilihoji.

Na mwisho kabisa, wanadiplomasia wnaona suala hilo la ajabu kwa Umoja wa ulaya kujumuisha baadhi ya nchi na nyingine kuzitenga.

Wageni kutoka Canada, Japan na China wanaweza kuruhusiwa kuingia kuanzia Julai, Mosi – kama China itaruhusu wageni wa Muungano wa Ulaya kuingia nchi kwake lakini sio kwa wageni kutoka Marekani.

Baada ya siku kadhaa za kujadiliana, orodha ya mwisho imeweza kujaribu kuonyesha ushiririkiano.

Orodha hii ya mwanzo inatarajiwa kuwa na uwezekano wa kufanyiwa maboresho kila wakati .

Ripoti ya wiki iliyopita ilisema mataifa wanachama wanachujwa katika orodha mbili tofauti.

Mtandao wa kisiasa umesema kuwa maambukizi kidogo chini ya 16 ya visa vya Covid-19 kwa watu 100,000 na wengine kesi 20, ambayo itajumuisha Canada na Uturuki.

Marekani imesema kuwa inabidi orodha hiyo wafanyie marekebisho kila baada ya wiki mbili ili Marekani pia iwepo katika orodha hapo baadae.

Mapema mwezi huu, tume ya ulaya iko katika mkakati wa kufungua mipaka kwa mataifa ambayo sin chi wanachama wa Umoja wa Ulaya magharibi mwa Balkans, nia ilikuwa kufungua kuanzia Julai, mosi.

Hata hibvyo , nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya Croatia imetangaza kuwa siku ya Jumatano wasafiri kutoka Serbia, Kosovo, Bosnia North Macedonia watakaa karantini kwa siku 14-ili kujitenga wenyewe kwa sababu ya ongezeko la maambukizi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *