Virusi vya corona : Idadi ya enye maambukizi ya virusi Afrika Ksuini ni zaidi ya nusu milioni


Afrika Kusini ndio nchi iliyoathiriwa zaidi na maambukizi ya Covid-19 barani Afrika

Maelezo ya picha,

Afrika Kusini ndio nchi iliyoathiriwa zaidi na maambukizi ya Covid-19 barani Afrika

M Zaidi ya watu nusu milioni wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Covid-19 nchini Afrika Kusini, kulingana na wizara ya ya afya nchini humo

Waziri Zwelini Mkhize ametangaza kuwa watu wapya 10,107 wamepatwa na maambukizi kwa siku moja tu ya Jumamosi, na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa na jumla ya watu 503,290 maambukizi ya virusi hivyo, pamoja na vifo 8,153.

Afrika Kusini ndio nchi iliyoathiriwa zaidi na maambukizi ya Covid-19 barani Afrika ambapo idadi ya maambukizi yake ni sawa na nusu ya maambukizi yote kwa ujumla yaliyoripotiwa katika nchi zote za Afrika.

Maelezo ya picha,

Rais wa Afrika Ksuini alisema nchi yake inakabiliwa na upungufu mkubwa wa wahudumu wa matibabu

Pia ni nchi ya tano yenye visa vingi zaidi vya maambukizi dunaini baada ya Marekani, Brazil, Urusi na India.

Maafisa wa wizara ya afya nchini Afrika Kusini wamesema kuwa viwango vya maambukizi vinaongezeka kwa kasi kubwa mno, huku watu wengi wanaopata maambukizi hayo kwa sasa wakiwa ni wakazi wa mji mkuu.

Zaidi ya theluthi moja ya maabukizi yameripotiwa katika jimbo la Guateng ambalo kwa sasa ni kitovu cha mlipuko nchini humo.

Maambukizi hayo hayatarajiwi kuongezeka kupita kiwango hicho, wanasema maafisa wa afya.

Afrika kusini iliweka amri ya kutotoka nje miezi ya Aprili na Mei Sambayo ilipunguza kusambaa kwa virusi vya corona.

Maelezo ya picha,

Afrika Ksuini inahangaika na mlipiuko mkubwa zaidi barani Afrika

Ilianza kufungua shughuli za kiuchumi taratibu mwezi Juni lakini masharti yaliyowekwa – iliwa ni pamoja na kupiga marufuku mauzo ya pombe- yalirejeshwa tena nwezi uliopita baada ya idadi ya maambukizi kuongezeka tena. Hali ya dharura pia imetangazwa kuanzia tarehe 15 Agosti.

Kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa kupita kiwango cha uwezo wa hospitali nchini humo pia ni mzigo mkubwa kwa hospitali na taarifa ya uchunguzi ya BBC ilibaini kushindwa kwa mfumo wa afya kwa ujumla jambo ambalo limewafanya wahudumu wa afya kufanya kazi ya ziada na hivyo kuchokana kuufanya mfumo mzima kukaribia kuvunjika.

Maelezo ya picha,

Afrika Kusini ilipiga marufuku uuzaji wa pombe ili kuzuwia usambaaji wa virusi vya corona , na polisi huwaadhibi wanaokamatwa wakinywa pombe

Mwezi uliopita rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa alisema kuwa vitanda 28,000 vya hospitali vimepatikana kwa ajili ya wagonjwa wa Covid-19 lakini nchi bado inaklabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari na wauguzi/ manesi

Wiki iliyopita Shirika la Afya Duniani- WHO lilionya kuwa inachoitokea Afrika Kusini huenda ikawa ni dalili za kile kitakachotokea kote barani Afrika.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *