Virusi vya Corona: Idadi ya vifo 500,000 Marekani 'ni hatua ya kuumiza sana' asema Biden


Rais wa Marekani Joe Biden
Maelezo ya picha,

Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani, Joe Biden amehutubia taifa baada ya kurekodi vifo 500,000 vilivyotokana na virusi vya corona, idadi kubwa zaidi kufikiwa ulimwenguni.

”Kama taifa, hatuwezi kukubali mwisho huu mbaya. Tunapaswa kuepuka kufa ganzi kwa huzuni,” alisema.

Rais na Makamu wa Rais , na wake zao, kisha walikaa kimya nje ya White House wakati wa tukio la kuwasha mshumaa.

Zaidi ya Wamarekani milioni 28.1 wamepata maambukizi ambayo pia ni idadi ya juu zaidi duniani.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *