Virusi vya corona: Warundi waliokwama Dubai wanaililia serikali yao iwarejeshe nyumbani


Wengi miongoni mwa Warundi waliokwamba Dubai ni vijana waliokwenda kutafuta ajira Dubai

Maelezo ya picha,

Wengi miongoni mwa Warundi waliokwamba Dubai ni vijana waliokwenda kutafuta ajira Dubai

Warundi zaidi ya 200 waliokwama katika mjini Dubai katika Muungano wa nchi za kiarabu tangu mwezi Machi mwaka huu wakati safari za ndege za kimataifa zilipofungwa kutokana na virusi vya corona wanasema wameshindwa kuondoka mjini humo.

Wanasema wako katika hatari ya kufungwa jela baada ya muda wa mwisho wa kuishi mjini humo waliopewa na serikali ya Emirate utakapoisha tarehe 12 Agosti.

Wanasema walikua wamelipia tiketi za safari zao za kurejea nyumbani katika kampuni ya ndege ya Kenya -Kenya Airways, lakini wanasema kuwa kampuni hiyo iliwaambia kuwa haiwezi kusafirisha ndege zake nchini Burundi kwasababu Uwanja wa ndege wa Burundi bado umefungwa.

Ubalozi wa Burundi mjini Dubai umesema kuwa tatizo lao linashughulikiwa na kwamba litapatiwa ufumbuzi hivi karibuni.

Mmoja wa Warundi hao Banga Rigumye, ambaye alikwenda Dubai kutafuta kazi , ameiambia BBC kuwa matatizo waliyonayo yalianza tangu mwezi Machi mwaka huu, baada ya Burundi kufunga uwanja wake wa ndege..

“Tulikua tumejiandaa tarehe 22 machi kuondoka Dubai…siku hiyo hiyo serikali ya Burundi ikatangaza kuwa uwanja wa ndege umefunga wakati hapa Dubai tangazo lililkua limetolewa kuwa uwanja wa ndege ungefungwa tarehe 25 mwezi Machi “.

“Sisi tulikua tumejiandaa kupanda ndege tarehe hiyo ili Dubai wasitufungie uwanja kabla hatujatoka “.

Bwana Rigumye anasema kuwa waliukimbilia ubalozi ili uwasaidie waondoke, lakini hawakufanikiwa.

Anasema serikali ya Muungano wa nchi za kiarabu ilikua imekubali kuwapatia vibali vya kukaa nchini humo ambavyo vingemalizika mwezi Disemba, lakini baadae ikabadilisha uamuzi huo.

” Tulitangaziwa kuwa kufikia tarehe 12 Agosti tuwe tumeondoka Dubai, la sivyo anayeweza alipe dola 700 ili apewe kibali kipya (visa). Tatizo tulilonalo sisi Warundi kutokana na virusi vya corona hatuna kazi za kutuwezesha kupata pesa hizo wanazotomba.”, Rigumye ameiambia BBC.

Anasema kuwa iliwabidi Warundi hao waishi Dubai bila kazi ,hadi wenye nyumba wakaanza kuwafukuza na baadhi yao wanashinda na kulala nje , “Chakula kupata ni bahati”.

Wameiomba serikali ya Burundi kuwasaidia kurejea nyumbani hata kabla ya kufungua rasmi uwanja wa ndege, kabla ya serikali ya Muungano wa nchi za kiarabu haijawachukulia hatua za kisheria.

Eddy Kevin Gahire ni muwakilishi wa Warundi wanaoishi Emirate ambaye anasema walifahamishwa kuhusu hilo na wao wakalifikisha katika ubalozi wa Burundi mjini Dubai.

Balozi wa Burundi katika Muungano wa nchi za Kiarabu ameafiki kuwa anawatambua Warundi hao na akazema anafanya kila liwezekanalo ili tatizo lao lipatiwe ufumbuzi.

Bapfinda Epimeni aliiambia BBC kuwa tatizo hili pia limewakumba Warundi walio katika mataifa mengine , lakini tatizo la Warundi waliopo Dubai ni vijana wa kike na kiume waliokwenda kutafuta ajira ndogondogo.

“Wana tatizo tena kubwa sana kwasababu wengi wao hawana hata mala pa kulala, wengi hawana uwezo wa kupata hata chakula “.

” Wanachokiogopa sasa ni kwamba serikali ya nchi hii ilitangaza hivi karibuni kwamba yeyote atakayepatikana akiwanchini humu baada ya tarehe 12 Agosti atachukuliwa kama mtu anayeishi hapa kinyume cha sheria kulingana na sheria ya nchi hii “, alisema Balozi wa Burundi katika Muungano wa nchi za kiarabu Bapfinda Epimeni.

“Utakapofika wakati huo wataanza kulipishwa pesa za Emirate -Durham 100 , wakatuhawana uwezo wa kupata hata pesa za chakula “. Aliongeza.

Bapfinda Epimeni, Balozi wa Burundi katika Muungano wa nchi za kiarabu, anasema analifahamu.

Maelezo ya picha,

Bapfinda Epimeni, Balozi wa Burundi katika Muungano wa nchi za kiarabu, anasema analifahamu tatizo la Warundi waliokwamba Dubai na analishughulikia

Balozi Epimeni anasema kile walichokifanya ni kuwaandikia barua maafisa wa Burundi, kuwafahamisha juu ya masaibu wanayopitia na akasema wamewajibu na wakauomba ubalozi uandike orodha ya Warundi wanaotaka kurejea nyumbani kutoka Dubai. Anasema ana matumaini kuwa siku zijazo tatizo lao litapatiwa ufumbuzi.

Amewaomba kuendelea kuwa wavumilivu na kusubiri hadi pale uwanja wa ndege wa Burundi utakapofunguliwa ili waweze kurejea nyumbani kwasababu walikua tayari wamelipa nauli ya ndege

Amewaambia kuwa iwapo tarehe 12/08 itafika kabla uwanja wa ndege wa Burundi haujafunguliwa atawaombea msamaha kwa Wizara mambo ya kijeni ya Muungano wa nchi za kiarabu ili wasitozwe faini.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *