Virusi vya corona: Watanzania waanza maombi ya siku 3 kumshukuru Mungu kwa kuwaepusha na janga


Magufuli

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Rais Magufuli alitoa ushauri kwa Watanzania kutumia siku tatu, kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili wiki hii kumshukuru Mungu kwa kuitikia maombi ya kuliepusha taifa na janga la Covid-19.

Raia wa Tanzania hii leo wanaanza siku tatu za maombi ya kumshukuru Mungu baada ya Rais wa nchi hiyo John Magufuli kusema maambukizi ya Covid-19 nchini humo yamepungua.

Hii inafuatia ushauri wa Rais John Pombe Magufuli alioutoa alipokuwa wilayani Choto mwishoni mwa juma aliwataka raia wa Tanzania kutumia siku tatu hizi, kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili wiki hii kumshukuru Mungu kwa kuitikia maombi ya kuliepusha taifa na janga la Covid-19.

”Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 …Ijumaa, Jumamosi na Jumapili KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia”, Magufuli.

Hata hivyo, katika kipindi hiki ambacho serikali imeacha kutoa takwimu za kila siku, ni vigumu kwa watu kujua ni kwa kiasi gani maambukizi hayo yamepungua nchini.

Viongozi wa upinzani pamoja na wakosoaji wa serikali ya Magufuli wameendelea kuwataka Watanzania kuchukua tahadhari za kujiepusha na maambukizi ya virusi vya corona.

Akijibu ujumbe wa twitter wa rais Magufuli uliowataka Watanzania kuanza siku siku tatu za maombi ya kumshukuru Mungu kwa kuiepusha Tanzania na janga la Corona, Kiongozi wa upinzani nchini humo na Mbunge Bwana Zitto Kabwe ambaye amekua akitilia shaka kupungua kwa maambukizi nchini humo, aliwataka Watanzania kujiepusha na mikusanyiko:

Serikali ilisitisha utangazaji wa takwimu za ugonjwa huo mara kwa mara mwezi Aprili baada ya rais kulalamika kwamba desturi ya kutangaza idadi ya wagonjwa ilikuwa inaongeza hofu. Alisema ilifaa pia maafisa kuangazia waliokuwa wanapona ugonjwa huo.

Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Umoja wa Afrika wiki iliyopita kilitoa wito kwa Tanzania kutoa takwimu na kwa wakati.

Nchini Tanzania pia Freeman Mbowe mkuu wa chama cha upinzani CHADEMA, awali alitilia shaka kupungua kwa maambukizi ya Covid -19, akisema taifa halina takwimu na mipango ya kukabiliana na mlipuko wa virus:

Haki miliki ya picha
CHASDEMA/Twitter

Hata hivyo licha ya miito ya viongozi wa upinzani, Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji hilo la kibiashara ambao ni takriban milioni sita kujitokeza na kusheherekea mwisho wa Corona ifikapo siku ya Jumapili

Hatua ya Bwana Makonda inaonekana kukiuka miongozo ya Wizara ya afya pamoja na shirika la afya duniani ya kuweka umbali baina ya mtu na mtu ikiwa ni moja wapo ya hatua za kudhibiti kuenea kwa maambukizi.

”Wenye mahoteli,wenye mabaa, makampuni na biashara zote turudi kazini. Ifikapo Jumapili kila mmoja apige shangwe na kila aina ya fujo ikiwa ni ishara ya kwamba Mungu wetu ametushindia. Washa muziki wako, siku hiyo nimekupa uhuru,piga sherehe ”, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo akisema.

Dar es Salaam ni moja ya miji yenye idadi kubwa ya watu ikikadiriwa kuwa na wakazi takriban milioni sita na idadi ya watu walioambukukizwa ni kubwa zaidi kuliko mikoa mingine nchini humo.

Tayari kuna jumbe zimeanza kutolewa kupitia mitandao ya kijamii kuhamasisha watu kujumuika kwa sherehe katika jiji kuu la biashara la Dar es Salaam.

Haki miliki ya picha
Mitandao ya kijamii

Image caption

Mmojawapo ya jjumbe ambazo zimekua zikiwatolea wito watu kukusanyika kwa sherehe jijini Dar es Salaam kupitia mitandao ya kijamii

Wakati huo huo, Serikali ya Tanzania imetangaza kufunguliwa kwa vyuo na michezo.

Raia wa Tanzania wameendelea kuwa na hisia tofauti juu ya rais Magufuli na serikali yake kutoa hakikishi kuwa maambukizi ya virusi vya corona nchini humo yamepungua. Baadhi wanaamini kauli za Magufuli na serikali yake huku wengine wakiendelea kuhoji ukweli wa kauli hizo kutokana na kwamba ni muda mrefu serikali haitoi taarifa kuhusu ugonjwa wa corona kama ilivyo kwa mataifa jirani.

Wasi wasi huo pia unatokana na kwamba tayari mataifa jirani yamefunga mipaka na Tanzania na kurushusu safari za malori ya mizigo pekee.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena

Vitu vinne unavyohitaji kuwa navyo wakati huu wa coronaSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *