Virusi vya corona: Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania yafanya mazungumzo na Kaimu balozi wa Marekani


Image caption

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Imni Peterson

Wizara ya Mambo ya Nje nchini Tanzania hii leo imefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini humo ili kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa kuhusu taarifa za ugonjwa wa corona ambao ubalozi huo umekuwa ukizitoa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka wizarani, Kaimu Balozi Imni Peterson amefanya mazungumzo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Wilbert Ibuge.

“…Katibu Mkuu ameeleza masikitiko yake kutokana na namna ambavyo Ubalozi huo umekuwa ukitoa taarifa mbalimbali za ushauri wa kiusafiri (travel advisory) zinazoandikwa na kusambazwa na Ubalozi wa Marekani kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo suala la namna ambavyo Tanzania inashughulikia ugonjwa wa Covid-19,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Wizara hiyo imepigia mfano wa taarifa za tarehe 13 na 25 Mei ambazo ziliwalenga raia wa Marekani waishio Tanzania ama wanaotaraji kwenda nchi hiyo.

“Tahadhari hizo zimeendelea kudai kuwa hospitali nyingi jijini Dar es Salaam (bila ya kuzitaja hospitali hizo) zimefurika wagonjwa wa COVID-19 jambo ambalo siyo kweli na linauwezekano wa kuzua taharuki kwa Watanzania na wageni kutoka nje ya nchi…”

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wizara imemtaka kaimu balozi kutoa taarifa zilizothibitishwa na kuwa hakuna kizuizi serikalini kwa mabalozi kupata “taarifa sahihi na zenye ukweli.”

Hata hivyo, taarifa hiyo haijanukuu maelezo ya Kaimu Balozi kwenye mkutano huo, na ubalozi wa Marekani pia haujasema lolote kwenye mitandao yake ama tovuti kuhusiana na mkutano huo.

Ubalozi wa Marekani umetoa tahadhari gani?

“Hatari ya kupata maambukizi ya Corona jijini Dar es Salaam ni kubwa sana. Licha ya kwamba taarifa hazitolewi mara kwa mara.

Ushahidi wote unaonyesha kuwa kuna mlipuko mkubwa wa maambukizi ya corona jijini Dar es Salaam na meneo mengine ya Tanzania. Ubalozi wa Tanzania unawataka raia wa Marekani pamoja na familia zao kubaki nyumbani na kutoka kwa ajili ya mahuitaji muhimu tu kama chakula, na kuzuia kukaribisha wageni katika nyumba zao,” ilieleza sehemu ya tahadhari ya Mei 13.

Na katika taarifa ambayo imetolewa jana ubalozi huo umesisitiza kuwa hospitali jijini Dar es Salaam zimeelemewa na wagonjwa na taarifa za takwimu rasmi za mwenendo wa ugonjwa huo hazijatolewa toka Aprili 29.

Pia unaweza kusoma:Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *