Virusi vya corona: Zaidi ya watu milioni moja wameathirika duniani


Wauguzi

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Wahudumu wa afya wameonekana kuzidiwa kazi zao za kutoa huduma kwa wagonjwa

Zaidi ya watu milioni moja wamethibitishwa kuathirika na virusi vya corona, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chuo cha Johns Hopkins.

Karibu watu 53,000 wamepoteza maisha na watu 2,10000 wamepona kwa mujibu wa ripoti za chuo hicho.

Marekani ina watu wengi zaidi walioathirika , na zaidi ya watu 1,000 wamepoteza maisha.

Ugonjwa huu wa Covid-19 , uliibuka katikati mwa China miezi mitatu iliyopita.

Ingawa ripoti ya Johns Hopkins inaeleza kuthibitishwa kwa watu milioni moja, idadi inakisiwa kuwa kubwa zaidi.

Ilichukua mwezi mmoja na nusu kwa watu 100,000 kurekodiwa. Watu milioni moja walifikiwa baada ya wiki iliyopita kuwepo na watu walioambukizwa idadi mara mbili zaidi.

Karibu robo ya watu walioathirika na virusi wamerekodiwa nchini Marekani huku barani Ulaya karibu nusu ya waathiriwa.

Kinachoendelea

Siku ya Alhamisi Uhispania ilisema kuwa watu 950 wamepoteza maisha katika kipindi cha saa 24, baadae Marekani iliripoti zaidi ya vifo 1,000 katika kipindi cha saa 24.

Idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa nchini Uhispania ilipanda kutoka 102,136 siku ya Jumatano kufikia 110,238 – kwa asilimia 8 sawa na kiwango kilichorekodiwa siku zilizopita.

Mamlaka zinaamini kuwa maambukizi yameshika kasi na kuwa zinatarajia kushuhudia idadi ya wanaoambukizwa ikishuka siku za mbele.

Uhispania ni ya pili kwa kuathiriwa vibaya kutokana na idadi ya vifo, pia karibu watu 900,000 wamepoteza kazi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *