Vita vya Syria: Mashambulizi ya Israel yalenga ngome zenye kuhusishwa na Iran


File photo showing an Israeli F-35 fighter jet flying over southern Israel (27 June 2019)

Maelezo ya picha,

Israeli haijasema lolote kuhusiana na taarifa hizo lakini mara kwa mara imekuwa ikishambulia maeneo yenye kuhusishwa na Irani nchini Syria

Israeli imeripotiwa kufanya mashambulizi ya anga katika maeneo yanayosemekana kuwa ya waasi wanaoungwa mkono na Iran huko nchini Syria ikiwa ni shambulizi la nne la aina hiyo ndani ya wiki mbili.

Shirika la habari la Sana linalomikiwa na Syria limesema ndege za Israeli zilishambulia maeneo ya magharibi ya Deir al-Zour na Albu Kamal.

Taarifa hiyo haikusema kama kuna yeyote aliyejeruhiwa lakini Shirika la Haki za Binadamu la Syria lenye makao yake Uingereza limesema kuwa wanajeshi wa Syria 14 na waasi washirika wake 43 wameuawa kwenye shambulizi hilo.

Israeli haijasema lolote lakini mara nyingi hushambulia maeneo lengwa yenye kuhusishwa na Irani nchini Syria.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *