Vrusi vya corona: Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta atoa mipango ya kufua uchumi


Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza mipango ya kusaidia biashara na raia kusonga mbele katika kipindi hiki cha mdororo wa kiuchumi kwasababu ya janga la virusi vya corona

Rais ameutubia taifa kutoka Ikulu ya rais, Nairobi na kusema kwamba mipango hiyo itagharimu shilingi bilioni 53.7.

Aidha, rais amesema kuwa taifa hilo haliwezi kuendelea kuchukua hatua za kusalia ndani milele.

”Sisi kama serikali, kama serikali zingine, mataifa yote dunia zimeanza kuona, hatuwezi kuendelea kusema wakenya tukae nyumbani, hatuwezi kuendelea kusema tu wakenya msiende kufanya biashara, musiende makazi, namna hio. Lakini, ile kitu ambayo itatusaidia pia kwa kikamilifu kuhakikisha ya kwamba tumeweza tena kufungua uchumi wetu na wananchi waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida. Nimewaambia wenzangu, hii haitakuwa kwa sababu ya yale serikali itatenda, itakuwa kwa sababu ya yale kila mmoja wetu kwa kibinafsi atafanya.

Kenya inachukua hatua sawa na zile ambazo pia zimechukuliwa nan chi nyengine kama hatua ya kuchechemua uchumi unaoendelea kudidimia.

Uhuru amesema hayo wakati ambapo pia alitangaza kuwa Kenya imerekodi visa 31 vipya vya maambukizi ya virusi vya coona na kufikisha idadi hiyo kufikia 1192.

”mimi sina shaka Wakenya tukishirikiana, tuungane pamoja, tutashinda huu ugonjwa. Lakini tena leo wakati natoa hii hotuba ambayo tumetoa sasa ya kusema lengo mbali mbali ambayo serikali inachukua kurahisisha maisha ya wananchi wa kawaida na kuhakikisha ya kwamba wananchi bado wanaweza kuendelea na maisha yao kupitia hio stimulus package ambayo nimeitaja, lazima tukumbuke ya kwamba jukumu ni letu sisi sote.”

Alitoa wito kwa raia wa Kenya kwamba ikiwa wataendelea kutekeleza masharti yaliyowekwa bila shaka taifa hilo litafanikiwa kukabiliana na changamoto zilizopo kwa sasa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *