Waandamanaji waonyesha utulivu Portland wakati maafisa wa usalama wakiondolewaHilo linatokana na makubaliano yaliofikiwa ambayo maafisa wa Oregon wanatarajia yataendelea kupunguza mvutano wakati mji huo uliokuwa na ghasia za maandamano kwa miezi kadhaa ukijaribu kusonga mbele.

Maandamano ya Ijumaa usiku yalifanana na yale ya Alhamisi, ambapo kwa mara ya kwanza katika wiki kadhaa maandamano yalimalizika bila ya mapambano makubwa kati ya polisi na waandamanaji, uvunjifu wa amani na watu kukamatwa.

Kubadilika kwa hali nje ya jengo la mahakama na serikali kuu kitovu cha mapambano kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama wa serikali kuu ni hatua inayotokana na serikali ya Marekani kuanza kuondoa maafisa wake wa usalama kutoka mji huo wenye muelekeo wa siasa za kushoto, chini ya makubaliano yaliofikiwa kati ya Gavana Mdemokrat Kate Brown na Uongozi wa Trump.

Hadi usiku wa manane Ijuma, hakuna maafisa wa usalama wa serikali kuu waliojitokeza katika eneo la jingo la mahakama, mahali walipokuwa wanakutana waandamanaji kwa wiki kadhaa, na kulikuwa hakuna ishara ya kuwepo kwa wasimamizi wa usalama kulizunguka eneo hilo.

Uzio ambao ulikuwa unawatenganisha waandamanaji na maafisa wa usalama waliokuwa wamepelekwa eneo la jingo la mahakama ulikuwa umepambwa kwa mapulizo na bendera za Marekani zilizopinduliwa juu chini zikiunganishwa na michoro iliyokuwa juu yake na herufi “BLM”, ikimaanisha Maisha ya Mtu Mweusi Yanathamani.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *