Waandamanaji Zimbabwe wamepanga maandamano mengine leo


Waziri wa mambo ya nje na biashara ya kimataifa nchini Zimbabwe, Sibusiso B. Moyo ameutetea ukamataji uliofanyika Jumatatu kwa waandamanaji wanaoipinga serikali na alitoa wito kuwepo hali ya kustahmiliana katika kipindi hiki cha kurejesha uchumi wa nchi hiyo ulioharibika.

Moyo aliiambia Sauti ya Amerika-VOA wakati wa mahojiano kwamba japokuwa kila mtu ana haki ya kuandamana, kumekuwepo na kampeni nyingi zinazochochea ghasia na kukiuka usalama wa umma. Alikubaliana na mahakama ya Zimbabwe kuunga mkono marufuku iliyokwekwa na polisi kwa maandamano yaliyoandaliwa na ushirika wa upinzani wa Movement for Democratic Change-MDC.

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa

Viongozi wa ushirika wanamshinikiza Rais Emmerson Mnangagwa na chama chake tawala cha ZANU-PF kusimamia jukumu la serikali ya mseto. Maandamano mengine yamepangwa kufanyika Jumanne kati kati ya mji wa Gweru na mengine Jumatano huko kusini mashariki mwa mji wa Masvingo nchini Zimbabwe.

Awali viongozi hao walipanga maandamano ambayo yalipigwa marufuku Jumatatu na maafisa polisi huko Bulawayo, mji wa pili kwa ukubwa nchini ZimbabweSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *