Wanajeshi wauawa kutokana na shambulio la al-Shabab, Somalia


Kiasi watu 10 wameuwawa kwenye mapigano kufuatia shambulizi la kundi la kigaidi la Alshabab ndani ya kambi moja ya kijeshi nje kidogo ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Afsia wa ngazi ya juu wa jeshi la Somalia, Ahmed Guhad amesema wanajeshi wawili na mfanyakazi mmoja kutoka kituo cha radio cha jeshi ni miongoni mwa waliouwawa wakati wa shambulizi hilo, ambalo pia limewauwa wanamgambo 7 wa Alshabaab.

Guhad amesema wanamgambo wenye silaha waliivamia kambi ya jeshi kutoka pande tofauti baada ya mirupiko ya kutegwa kwenye magari katika kijiji cha Awdhegle, kilometa 70 kusini ya Mogadishu.

Kwa upande wake Al shaabab imesema kupitia kituo chake cha redio kuwa wamewauwa wanajeshi kumi wa Somalia wakati wa shambulzii hilo.

Chanzo: ReutersSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *