Wanamgambo wa Kiislamu walichinja watu 12 katika mji waliouvamia Msumbiji


Wanamgambo wa Kiislamu waliuteka mji wa Palma kwa siku 10
Maelezo ya picha,

Wanamgambo wa Kiislamu waliuteka mji wa Palma kwa siku 10

Miili ya watu 12, wanaokisiwa kuwa raia wa kigeni imepatikana ikiwa imekatwa vichwa katika mji wa Palma, Kaskazini Mashariki mwa Msumbiji, wakati mji huo ulipovamiwa na wapiganaji wa kiislamu mwezi uliopita, kamanda wa polisi wa eneo hilo ameiambia runinga ya serikali, shirika la habari la Reuters linaripoti.

Pedro da Silva aliwaonyesha waandishi wa habari mahali ambapo anasema kuwa aliizika miili hiyo 12.

“Walikuwa wamefungwa na kukatwa vichwa hapa,” alionekana akisema katika mkanda wa video uliorushwa na televisheni ya serikali jana Jumatano.

Alinukuliwa pia akisema kwamba aliamini watu hao 12 walikuwa wageni kwa sababu walikuwa wazungu, lakini hakuwa na uhakika wa mataifa yao.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *