Watafiti : Upandikizaji wa majimaji ya uke kuanza karibuni Marekani


Vijidudu vya BV vikiwa vimefunika seli

Haki miliki ya picha
Getty Images

Madaktari nchini Marekani wana matumaini kuanza kutoa mababu ya kupandikiza majimaji ya uke, na hivi sasa wameanza mipango ya kuwapata watu watakaojitolea kwenye programu hiyo.

Wanaamini baadhi ya wanawake wanaweza kunufaika na matibabu hayo kuwasaidia kuwalinda dhidi ya maambukizi yanayotokana na bakteria waitwao kitaalamu Bacterial Viginosis (BV)

Wataalamu kutoka chuo cha John Hopkins wanasema walivutiwa na mafanikio ya upandikizaji wa kinyesi. (Faecal transplant)

Ingawa dawa za kupambana na vijidudu zinaweza kutibu ugonjwa wa BV, mara nyingi ugonjwa huu hurudi tena.

BV ni nini?

BV si ugonjwa wa zinaa, ingawa ni ugonjwa wa kuambukiza.

Wanawake ambao hupata ugonjwa huu wanaweza kubaini kuwa wanatoka majimaji yasiyo ya kawaida ambayo yana harufu mbaya.

Ugonjwa huu unapaswa kutibiwa kwa sababu ugonjwa huu unaweza kuwafanya wanawake kuwa hatarini kupata magonjwa ya zinaa na kupata madhara kwenye mfumo wa mkojo.

Ikiwa mwanamke ni mja mzito, inaongeza hatari ya kujifungua mtoto kabla ya wakati.

Kwanini wanachora nyuso zao kwa damu ya hedhi?

Huwezi kusikiliza tena

Wasichana wanatumia vikopo vya hedhi kujisitiri

Maji maji hayo yatakuwa msaada kwa namna gani?

Sehemu za uke,kama kwenye tumbo kuna aina tofauti za vijidudu.

Aina za vyakula, mtindo wa maisha na aina ya dawa tunazotumika zinaweza kuathiri mfumo wa vijidudu.

Vijidudu kwenye sehemu za uke hupendelea mazingira yenye acid lakini inapokuwa na alkali nyingi vijidudu vingine vikiwemo vinavyosababisha BV huzaliwa.

Sababu kadhaa zinaweza kuinua pH ya uke na kufanya BV iweze zaidi, ikiwa ni pamoja na kufanya ngono (mbegu za kiume na mate ni alkali kidogo) pamoja na mabadiliko ya homoni wakati fulani wa mwezi wakati wa mzunguko wa hedhi wa mwanamke.

Upandikizaji utafanyikaje?

Watafiti wamekuwa wanatazamia kufanya majaribio hayo muda mfupi ujao baada ya kupata ruhusa ya mamlaka ya udhibiti wa chakula na dawa.

Walichunguza watu kadhaa na kutoa ripoti katika jarida la masuala ya afya.

Kutokana na uchunguzi walioufanya kwa wanawake 20, watafiti wanasema wamefahamu nani atafaa kujitolea kwenye programu hiyo

Kwa tahadhari, watakaofaa kutoa majimaji yao kwa ajili ya upandikizaji watatakiwa kuepuka kushiriki kimwili kwa takribani siku 30 kabla ya kutoa sampuli, na kuwa sampuli zao zitapimwa kuona kama zina maambukizi yeyote ikiwemo virusi vya ukimwi, ili kuepuka kusambaa kwa atakayepandikiziwa.

Mtafiti Daktari Laura Ensign, amesema hii ni programu ambayo watu watajitolea kwa hiyari.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *