Wazazi waandamana Uingereza kupinga masomo kuhusu mahusiano ya jinsia moja


Protestor holds a sign

Image caption

Waandamanaji walidai kuwa somo hili linaenda kinyume na dini ya kiislam na watoto wa shule msingi ni wadogo sana kujifunza kuhusu mahusiano ya jinsia moja.

Baadhi ya watu nchini Uingereza wameamua kuandamana nje ya shule kupinga mafunzo ya ushoga shuleni.

Wizara ya Elimu nchini humo imesema kwamba inafanyia kazi ghasia hizo ili mamlaka ziwe na taarifa zaidi na kuweza kuzisaidia shule.

Programu iitwayo ”No Outsiders equality” inahamasisha watoto kukubali utofauti kuhusu dini, familia na mahusiano.

Programu hiyo ilipitishwa mwezi Machi baada ya waandamanji wenye hasira kali kuandamana nje ya geti la shule ya umma ya Parkfield katika mji wa Birmingham.

Waandamanaji walidai kuwa somo hili linaenda kinyume na dini ya kiislamu na watoto wa shule msingi ni wadogo sana kujifunza kuhusu mahusiano ya jinsia moja.

Haki miliki ya picha
PA Media

Bodi ya walimu ilisema kuwa takriban shule 70 nchini Uingereza walishuhudia wazazi wengi ambao hawakubaliani na elimu hiyo ya mahusiano.

Nyaraka iliyoandaliwa na wizara ya elimu imetoa ushauri kwa mamlaka kuchukua hatua kwa sababu kama wazazi wakiamua kuwatoa watoto wao shuleni kwa kutokubaliana na kile kinachofundishwa wana haki.

Na kama maandamano yataendelea nje ya shule, basi walimu wakuu wachukue tahadhari na kuomba msaada wa polisi endappo waandamanji watavunja sheria.

Walimu walioona nyaraka hiyo wameiambia BBC kuwa hawajafurahishwa na kitendo cha kutoshirikishwa kuanzia mwanzo kuhusu kuanzishwa kwa somo hilo.

Elimu ya mahusiano itafudishwa kwa wanafunzi wote wa shule ya msingi kuanzia mwezi septemba 2020 ,”mashirika mengi hawakubaliani na uanzishwaji wa masomo hayo, au kwa kiwango ambacho kinatarajiwa kufundishwa.” Nyaraka hiyo iliyovujishwa ilieleza.

Haki miliki ya picha
Department for Education

Image caption

mfano wa barua ambao unaweza kutumika kwa wazazi kukataza mtoto wake kufundishwa masomo ya mahusiano

Watu wanaoishi katika mji wa Birmingham ndio wamekuwa wakionyesha pingamizi zaidi dhidi ya masomo hayo kwa kuendelea kuandamana nje ya shule.

Kesi iliyopo Mahakama kuu itatoa uamuzi kuhusu urejesho wa maandamano nje ya shule yaweza kuanza tena.

Wizara ya elimu imewafafanulia watu wanaofanya kampeni kuwa hawawezi kutofautisha kuhusu masomo yanayofundishwa shule na elimu ya mahusiano ambayo wana uamuzi wa kuchagua kukubaliana nayo au kutokubaliana nayo.

Haki miliki ya picha
PA Media

Image caption

Mamlaka za shule zimeshauriwa kuongea na vyombo vya habari kuhusu maandamano yoyote

Imeshauri kuwa shule zizungumze na wazazi kuhusu programu zao za elimu, lakini pia wafikirie kuhusu maoni ya wazazi.

”Ushauri huu umelenga kuhamasisha wazazi kuongea na shule kuhusu jambo lolote ambalo litakuwa linawatatiza, kuliko kuandamana nje ya shule jambo ambalo litasaidia mamlaka kuangalia njia mbadala”,wizara ya elimu imeeleza.

Hata hivyo serikali imeshauriwa kuziunga mkono shule zinazofundisha elimu ya jinsia moja kiundani zaidi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *