Waziri mkuu Boris Johnson akabiliwa na wakati mgumu


Mpango wake umeibua maoni mseto, baadhi ya raia wakisema anaiweka Uingereza katika hatari kubwa na wengine wakilalamika dhidi ya mikakati yake mikali katika kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Corona nchini humo.

Kwa muda mrefu, Boris Johnson amejulikana pakubwa kama mtu anayejisifu kuwa “ana uwezo mkubwa wa uongozi na ameiga mtindo wa utawala wa watangulizi wake” kama Winston Churchil, waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo.

Hata hivyo, Rob Mudge mwandishi wa DW, katika maoni yake anasema Johnson ameshindwa kuchukua hatua za moja kwa moja kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Corona, tofauti na Winston Churchil, waziri mkuu aliyetatutua na kuchukua hatua za haraka wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia alipokuwa akiiongoza Uingereza.

COVID-19 - Boris Johnson (Reuters/C. Recine)

Mwanaume akimfuatilia waziri mkuu Johnson wakati akizungumza na waandishi habari wakati mnamo wakati virusi vya Corona vikisambaa katika mji wa Newcastle, Machi 23, 2020.

Hali ya hatari? Hatari gani?
Hata hivyo raia wengi nchini humo wameshangazwa na hatua ya Johnson kuchukua mikakati mikali kupambana na Corona, ikiwemo kupiga marufuku ya watu kutokota ndani. Awali waziri huyo alisema Uingereza haitoweka mikakati hiyo kama ilivyo katika mataifa ya Ulaya ya Italia, Uhispania na Ufaransa ambako kuna maambukizi mengi ya virusi vya Corona.

Huenda Johnson amechukua hatua hiyo baada ya kugundua hatari kubwa ya virusi vya Corona, awali waziri huyo alisema virusi hivyo vilikuwa havijaenea kwa kasi nchini mwake. Lakini baadhi ya raia waliotaka waziri kutoa agizo la kusalia majumbani sasa wanalalamika dhidi ya kunyimwa uhuru wa kutembea.

Kwa sasa raia wanachokita kutoka kwa viongozi wao ni muongonzo na Ujumbe wazi lakini Borison ameshindwa kutekeleza hata moja kati ya hayo.

Wengi wanasema, waziri Johnson kutokuwa muwazi katika maneno yake huenda kutaisababaisha Uingereza kulipia gharama kubwa kutokana na hali ya janga a virusi vya Corona. Madaktari na wauguzi wametishia kuachia kazi kutokana na uhaba wa vifaa vya kujikinga wakati wa kuwatibu wagonjwa wa virusi hivyo. Rob Mudge anasema, wauguzi sasa huenda watalazimika kuamua kati ya ajira au usalama wa afya yao.

NSH UK - Coronavirus (Getty Images/Afp/D. Leal-Olivas)

Johnson katika moja ya harakati zake za kampeni alipotembelea hospitali ya King’s Mill mjini Mansfield, kaskazini mwa England.

Wafuasi wa Johnson wanasema waziri huyo ana haiba kubwa, lakini wengi wao wanamtaka aitumie pamoja na umahiri kuiongoza Uingereza kutoka katika hali ngumu kutokana na janga la Corona.

Mfululizo wa makosa
Boris Johnson anakabiliwa na janga kubwa zaidi katika kipindi chake cha uongozi kama waziri mkuu, wakati ambao utaamua haiba yake kama kiongonzi ni ipi?

Wakati wa uongozi wake kama waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, wadhfa wake ulikumbwa na makosa mengi ya kijinga ya kidiplomasia pamoja na kuteleza mara kwa mara.
Wakati mmoja, alimlinganisha rais wa zamani wa Ufaransa Francois Hollande kama mfungwa wa kambi ya vita, rais huyo alipotoa mtizamo wake kuhusu kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya.

NSH UK - Coronavirus (picture-alliance/dpa/D. Staples)

Waziri Mkuu Boris Johnson akikagua gari la kubeba wagonjwa alipozuru hospitali mjini Boston.

Rob Mudge anauliza swali balagha, iwapo raia wa Uingereza wanaweza kumuamini waziri mkuu kutatua janga walilonalo kwa sasa, waziri mkuu (Boris Johnson) ambaye alidai kuwa kanuni za usalama wa chakula katika Umoja wa Ulaya zilikuwa zikiigharimu pakubwa Uingereza ijapokuwa kanuni hizo ziliwekwa na Uingereza yenyewe.

Au waziri aliyefanya mpango wa kutumia pauni bilioni 20 kujenga daraja kuiunganisha Scotland na Ireland ya Kaskazini. Lakini kwa wakati huu serikali yake imetenga bilioni tano tu kugharamia shirika la kitaifa la huduma ya afya kama pesa ya dharura kukabiliana na Corona.

Mbali na kuangamiza maisha ya watu janga la virusi vya Corona litaiacha jamii ya Uingereza na alama isiyofutika kwa siasa na hali ya maisha ya raia wake. Rob Mudge anasema.

Chanzo: DW

 

 Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *