Waziri Mkuu wa Ukraine awasilisha barua ya kujiuzulu


Waziri Mkuu wa Ukraine Oleksiy Honcharuk ametangaza kujiuzulu na amefikisha rasmi kwa maandishi ombi lake hilo kwa Rais Volodymyr Zelenskiy siku ya Ijumaa (Januari 17). Waziri mkuu huyo amehudumu katika wadhifa huo katika muda wa chini ya miezi sita.

Kujiuzulu kwa waziri mkuu huyo wa Ukraine kumetokana na sauti iliyorekodiwa kwenye mkanda inayodaiwa kuibuka mapema wiki hii ambapo Honcharuk alisikika akihoji uwezo wa Zelenskiy katika kusimamia uchumi wa nchi hiyo jambo ambalo waziri mkuu ameliona kuwa linakiuka maadili ya wadhifa wake.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (picture-alliance/ZUMAPRESS/P. Gonchar)

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

 Kwenye ujumbe aliouandika kwenye Facebook, Honcharuk alisema kuwa nafasi aliyopewa ilikuwa na lengo la kutimiza programu ya Rais Zelenskiy na kwamba kiongozi huyo kwake ni mfano wa uwazi na heshima. Barua ya kujiuzulu waziri mkuu huyo wa Ukraine inasubiri kuidhinishwa na ofisi ya rais ambayo ilijibu kwamba wangeizingatia.

Kabla ya kuwa waziri mkuu, Honcharuk alikuwa wakili katika ofisi ya waziri mkuu na ndiye alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Ukraine mwenye umri mdogo. Alikuwa na miaka 35 alipochukua jukumu hilo mnamo Agosti 2019.

Chanzo:/p.dw.com/p/3WL9C

 

 Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *