Waziri wa Elimu Israeli apendekeza mpango wa kuwatibu wapenzi wa jinsia moja


Israeli Education Minister Rafi Peretz. Photo: 24 June 2019

Haki miliki ya picha
AFP/Getty Images

Image caption

Rafi Peretz aliteuliwa kuwa waziri wa elimu wa Israeli mwezi uliopita

Waziri wa Elimu nchini Israeli Rafi Peretz amesema kuwa anaamini “matibabu ya kuwabadili wapenzi wa jinsia moja” yanaweza kufanya kazi.

Kauli hiyo hata hivyo imepingwa vikali nchini humo.

“Naamini inawezekana,” Bw Peretz, ambaye ni kiongozi wa dini ya kiyahudi (rabbi) mhafidhina amekiambia kituo cha runinga cha nchi hiyo Channel 12 TV.

Pia amesema kuwa yeye binafsi “anauelewa mkubwa juu ya suala hilo (la matibabu)”.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ni miongoni waliopinga mpango huo akisema matamshi ya waziri huyo “hayakubaliki”.

Wanasiasa wengine na makundi ya kutetea wapenzi wa jinsia moja nchini humo pia yamepaza sauti ya upinzani juu ya mpango huo.

“Matibabu ya kuwabadili wapenzi wa jinsia moja” yamekuwa yakipingwa sehemu mbalimbali duniani.

Matibabu hayo hujaribu kubadili tabia na mwonekano wa mpenzi wa jinsia moja kwa njia za kisaikolojia na maombi ya kidini.

Waziri Peretz amesema nini?

“Naamini inawezekana kumbadili [mpenzi wa jinsia moja],” Bwana Peretz alidai siku ya Jumamosi.

“Naweza kukuhakikishia kuwa nina uelewa mpana wa jambo hili kielimu na nimelifanya pia mimi binafsi.”

Akaeleza namna ambavyo aliwahi kumsaidia mtu mmoja ambaye alimfuata na kumueleza kuwa ni mpenzi wa jinsia moja.

“Awali ya yote, nilimkubali alivyo. Nikamweleza vitu vya kumtia moyo. ‘Nilimwambia, tufikiri. Tusome. Na tulitafakari jambo hili kwa kina zaidi.’

“Lengo ni kwanza kumfanya yeye mwenyewe ajitambue ipasavyo… na baada ya hapo atafanya uamuzi.”

Baadae lakini akajaribu kusawazisha kauli zake kwa kusema, haukuwa mpango wake kulazimisha watoto ambao wanaonekana kuwa na tabia za wapenzi wa jinsia moja kupelekwa kwenye matibabu hayo, linaripoti gazeti la Jerusalem Post.

Upinzani wa ‘matibabu’ umetoka wapi?

Waziri Mkuu Netanyahu amesema: “Kauli za waziri wa elimu juu ya jamii ya wapenzi wa jinsia moja hayakubaliki kwangu na wala hayawakilishi msimamo wa serikali ninayoiongoza.”

Netanyahu amesema kuwa ameongea na Bw Peretz, ambaye ni mshiika wake wa kisisasa kutoka chama cha kihafidhina cha muungano wa mrengo wa kulia na kumueleza masikitiko yake juu ya kauli hiyo.

Nitzan Horowitz, ambaye anaongoza chama cha mrengo wa kushoto cha kiliberali cha Meretz , amesema “matibabu ya kuwabadili wapenzi wa jinsia moja” ni mpango hatari ambao hupelekea vijana kuchukua hatua kali ikiwemo kujiua.

Muungano wa wapenzi wa jinsia moja nchini humo, ufahamikao kama Aguda, unamtaka waziri huyo ajiuzulu kutokana na matamshi yake hayo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *