White House yasema haitashiriki uchunguzi wa kumuondoa TrumpWakili wa White House Pat Cipollone ametuma barua yenye kurasa nane kwa viongozi wa Chama cha Demokrati katika Baraza la Wawakilishi, akiwemo Spika Nancy Pelosi, ambao wanaangalia iwapo Trump alivunja sheria kwa kuhimiza Ukraine kumchunguza mgombea urais wa chama cha Demokrat Joe Biden.

Cipollone anawashutumu Wademokrat kwa kuvunja “msingi wa uadilifu na ufuataji sheria uliowekwa na katiba.”

Anasema wanamnyima Trump nafasi ya kuwahoji mashahidi na kuona vidhibiti wanavyotumia kuamua iwapo aondolewe madarakani.

“Yote haya yanakiuka Katiba, utawala wa sheria, na kila utaratibu uliokuwepo huko nyuma,” Cipollone ameeleza kwa maandishi, akiongeza kuwa uchunguzi huu hauna msingi wowote, ni wa upande mmoja, na ni jaribio la kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais 2016.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *