Wolves 1-1 Man Utd: Paul Pogba akosa penalti ugenini


Paul Pogba (kushoto)

Haki miliki ya picha
PA Media

Image caption

Paul Pogba (kushoto) amekosa penalti nne akiicxhezea man United katika ligi ya Premia tangu mwanzo wa msimu uliopita

Penalti iliopigwa na kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba iliokolewa huku Man United ikizuiwa na Wolveshampton katika mechi ya kusisimua.

Huku ikiwa magoli 1-1 katika kipindi cha pili , raia huyo wa Ufaransa alichezewa visivyo na Conor Coady na kupewa penalti hiyo kuipiga licha ya kukosa penalti tatu msimu uliopita huku Rashford akifunga goli moja dhidi ya Chelsea katika mechi ya ufunguzi wikendi iliopita.

Shambulio hilo la pogba lilipanguliwa na Rui Patricio ambaye aliruka upande wake wa kulia.

Katika kipindi cha kwanza kilichoshirikisha mashambulizi matatu , Anthony Martial alikuwa ameiweka kifua mbele Man United akiifungia klabu hiyo goli lake la 50 – kabla ya Ruben Neves kusawazisha kupitia shambulio kali karibu na eneo la hatari dakika 10 baada ya kipindi cha kwanza.

Kichwa cha mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez kiligonga mwamba wa goli kabla ya Neves kufunga lakini hakuna kipa aliyevamiwa na mashambulio baada ya Pogba kukosa penalti hiyo.

Wakati mzuri na mgumu wa Martial

Haki miliki ya picha
Rex Features

Image caption

Anthony Martial amefunga magoli 36 ya ligi ya Premia akiichezea Manchester United miongoni mwa magoli 50

Akizungumza na vyombo vya habari siku ya Ijumaa, mkufunzi wa United Ole Gunnar Solskjaer alisema kwamba anamtaka Martial na Rashford kufunga magoli wanapokaribia lango la upinzani.

Pengine alikuwa akizungumzia kuhusu krosi iliopigwa na Rashford karibu na mwamba wa goli katika kipindi cha kwanza.

Martial hakusukuma mguu wake mbali na kushikana na beki huyo huku fursa hiyo ya wazi ikipotea.

Kilichofuatia ni magoli mangapi ambayo raia huyo wa Ufaransa anaweza kufunga iwapo atafuata mkondo huo wa kuwa hatari mbele ya lango.

Baada ya dana dana nzuri ilioanzishwa na Jesse Lingard akiwemo Luke Shaw na kumaliziwa na Rashford aliyepiga kombora la chini chini na kupita safu ya ulinzi ya Wolvehampton, Martial alipiga mkwaju kwa haraka huku kipa wa klabu hiyo akikosa nafasi ya kuokoa mkwaju huo.

Ulikuwa wakati mzuri kwa wageni hao ambao waliathiriwa na kupewa kadi ya njano kwa Daniel James kwa kujiangusha.

Kipindi cha pili ilikuwa hadithi tofauti lakini United pengine ingeibuka mshindi iwapo Pogba angefunga penalti hiyo.

Swali kuu ni kwamba ni kwa nini Pogba aliipiga penalti hiyo?

Baada ya kufunga dhidi ya Chelsea , Rashford pia alifunga penalti ya dakika za mwisho na kuipatia ushindi timu yake dhidi ya PSG msimu uliopita mbali na kufunga penalti ya England dhidi ya Colombia katika kombe la dunia la 2018.

Katika kipenga cha mwisho , Pogba alijifunika kichwa chake na tishati yake alipokuwa akitoka uwanjani.

Traore alibadilisha mchezo

Haki miliki ya picha
Rex Features

Image caption

Magoli 10 kati ya 13 ya Ruben Neves katika mashindano yote yalitoka nje ya eneo hatari

Juhudi za Martial baadaye zilibainika kuwa mkwaju wa pekee uliolenga goli katika kipindi cha kwanza dhidi ya mashambulizi matatu yaliolenga goli.

Wolves nao walifanikiwa kufanya mashambulizi mawili pekee katika goli.

Baada ya kuwashinda mara mbili msimu uliopita katika uwanja wa Molineux Wolves walikuwa wanapanga kupata ushindi wa tatu dhidi ya miamba hiyo ya Old Trafford kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 40.

Baada ya kipindi kibaya cha kwanza kuingizwa kwa Adama Traore kulibadilisha mechi hiyo.

Kasi ya Traore iliichanganya safu ya ulinzi ya United huku Wolves wakipata mkwaju wa adhabu kufuatia fauli ya beki Harry Maguire dhidi ya raia wa Uhispania Jimenez uliogonga mwamba wa ndani wa goli.

Hatahivyo bao hilo lilibadilika na kuwa ‘afueni kwa United baada ya Moutinho kumpata Neves wakati alipopiga krosi yake.

Katika benchi , mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo aliruka kwa furaha. David De Gea hakuweza kuona shambulio hilo lililomuacha mdomo wazi.

Bao hilo hatahivyo lilichunguzwa na refa msaidzi wa Video wa VAR kabla ya refa kuliidhinisha.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *