Zanzibar na kitendawili cha mrithi wa Maalim Seif


  • Rashid Abdallah
  • Mchambuzi, Tanzania

Maalim Seif

Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kwa sasa wameelekeza macho na masikio kwa raisi wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi wakisubiri amtangaze Makamu wa Kwanza wa Rais wa visiwa hivyo.

Tayari uongozi wa chama cha ACT Wazalendo umeshapendekeza jina la mwananachama wake atakayerithi nafasi hiyo iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha Maaalim Seif Sharif Hamad.

Baada ya hatua hiyo, inategemewa rais Mwinyi kumteua rasmi kiongozi huyo kama inavyobainisha Katiba ya Zanzibar katika ibara ya 40 (1).

Tarehe 17 Febuari, Rais Dkt. Hussein Mwinyi alitangaza kifo cha makamu wake wa kwanza, Maalim Seif Sharif Hamad kupitia runinga ya taifa ya ZBC. Kifo hicho kilikuja takriban wiki tatu tangu Maalim atangaze kuugua Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19).Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *