Abigail Chamungwana: Mwanamuziki mwenye umri mdogo aliye na ndoto ya kuwa Daktari bingwa wa upasuaji moyo wa watoto


Abigail

Haki miliki ya picha
Abigail

Image caption

Msanii Abigail Chamungwana

Ni kawaida kwa mtu yeyote anayetamani kutimiza ndoto zake kuweka nguvu zake zote kweye lile ananlotamani ili liweze kutimia.

Wengi huweka jitihada za ziada na hata kutafuta usaidizi zaidi ili tu kua na weledi wa jambo analotaka kulifanikisha.

Msanii Abigail Chamungwana akiwa na miaka kumi na sita pekee , amefanikiwa kutoa Albam na kutwaa tuzo kubwa Afrika Mashariki ya Maranatha.

Pamoja na jitihada anazoziweka kwenye muziki, Abigail ana ndoto ya kuwa Daktari Bingwa wa Upasuaji wa moyo kwa watoto.

Haki miliki ya picha
Abigail

Image caption

Mbali na kuwa mwanamuziki Abigail ana ndoto ya kuwa Daktari bingwa wa moyo wa watoto

Abby anasema ndoto yake ya kuwa Dakari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto ilianza wakati mmoja alipokua akisafiri aliona mtoto mdogo akisafirishwa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya moyo na pale katika umri ule mdogo alitamani sana akimaliza masomo yake awe daktari ili aweze kuwasaidia watoto wadogo.

”Mama aliniambia hakukua na madaktari wakati ule nchini Tanzania,niliumia sana kwakua mtoto alikua ni mdogo sana,lakini mpaka leo bado nina ndoto hiyo hiyo na muziki pia naendelea kufanya .”

Kwa sasa yupo katika masomo yake ya kidato cha tano na huko anasomea masomo ya sayansi yaani Fizikia,Kemia ,Biolojia na Hesabu,Lakini anasema wasichana wengi kama yeye wanaona ni masomo magumu lakini kwake sio kabisa kwani anataka kukamilisha ndoto yake.

Haki miliki ya picha
Abigail

Image caption

Wazazi wamekuwa wakimuunga mkono katika safari yake ya muziki tangu walipogundua kipaji chake

Abigael anamudu vipi kazi za muziki na masomo?

Anasema: ”Ninafanya muziki, nina masomo pia lakini nimeshatoa albamu yangu ya kwanza, Nimejipangia muda wangu vizuri hivyo naweza masomo na muziki vyote kwa pamoja ”

Abby anasema wazazi wake Baba na mama ndio wanaomsimamia katika kazi zake za kimuziki.

”Tuliona kipaji chake mapema,mimi na baba yake tukaona ni vizuri tukakuza kipaji chake na aweze kuendelea na masomo vizuri.Tulikua tunamsimamia zamani lakini kwa sasa ameshakua na ana miaka 16 sasa hivyo anajisimamia mwenyewe” Alizema mama yake Abigail.

Kuhusu namna walivyogundua kipaji chake mama yake anasema yeye na baba yake walikuwa wakimuona anacheza na wanasesere akiwaimbia.”Ni vizuri kukuza kipaji cha mtoto kwani kila mtoto anazaliwa na kipaji chake sisi tuliamua kufanya uwekezaji kwenye kipaji chake cha uimbaji”. Alimaliza mama Abigail.

Unaweza pia kusoma

Mtoto wa miaka 9 kutunukiwa shahada

Mtoto wa miaka 12 adahiliwa Chuo KikuuSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *