Afisa wa juu wa Shirikisho la Soka Nigeria ahojiwa kwa madai ya ubadhirifu wa pesa


The Nigeria Football Federation logo

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Shirikisho la Soka Nigeria limekanusha kujihusisha na vitendo vyovyote vya ufisadi

Makamu rais wa Shirikisho la soka nchini Nigeria, Seyi Akinwunmi ameachiliwa na wapelelezi wa Tume ya Kupambana na Ufisadi baada ya kuhojiwa kuhusu sakata ya kupotea kwa pesa.

Uchunguzi huo unaofanywa na Tume ya Kupambana na Uhalifu wa Kiuchumi na Fedha inachunguzi madai chungu nzima ya ufisadi kuhusu vile pesa zilizokusudiwa kufadhili mpira na maendeleo hazijulikani zilipo kulingana na tume hiyo.

Akinwunmi, Mkuu wa bodi ya soka mji wa Lagos amethibitisha kwamba amehojiwa kuhusu maswala ya fedha na kuachiliwa huru bila kupatikana na makosa yoyote.

“Nimehojiwa pamoja na wengine wengi kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea,” Akinwunmi, ambaye kila wakati amekuwa akikanusha kuhusika na sakata hiyo, amezungumza na BBC Michezo hii Jumamosi.

Uchunguzi kuhusu madai ya ufisadi umekuwa ukifanywa katika kipindi cha miaka miatatu iliyopita huku maafisa wengine wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo wakihojiwa pia. Hata hivyo wamekuwa wakikanusha madai hayo.

Katika miezi ya hivi karibuni, shirikisho la Soka Nigeria limekuwa likifuatiliwa kwa karibu ama iwe uwanjani au vyenginevyo.

Serikali ya Nigeria ilitupilia mbali madai ya ufisadi dhidi ya maafisa wengine watano wanaosimamia soka akiwemo Rais Pinnick mnamo mwezi Novemba.

Lakini Tume ya Kupambana na Ufisadi na mashirika mengine bado yanaendelea kuwachunguza.

Septemba 2019, Tume hiyo ilizuia mali ya baadhi ya maafisa waandamizi kama sehemu ya uchunguzi lakini bado haijafungua kesi rasmi dhidi ya shirikisho hilo au mwanachama wake yeyote.

Shirikisho la Soka Nigeria limekuwa likilaumu uchunguzi unaoendeshwa na tume hiyo kwa matokeo mabaya ambayo tume ya taifa imekuwa ikipata katika ngazi ya kimataifa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *