''Afueni'' kw awahamiaji 150 baada ya kuondoshwa Libya


Walioondoshwa Libya ni raia kutoka mataifa ya Eritrea, Ethiopia, Sudan

Haki miliki ya picha
UNHCR

Karibu wakimbizi na wahamiaji 150 wamesafirishwa kwa ndege kutoka mji mkuu wa Libya Tripoli, kuelekea katika mji mkuu wa Italia,Rome, na Shirika la Umoja wa Mataifa la huduma kwa wakimbizi UNHCR.

Wale waliochukuliwa ni raia kutoka mataifa ya Eritrea, Ethiopia, Sudan na na wengi wanahitaji matibabu na wanakabiliwa na utapiamlo.

Miongoni mwao ni watoto 65 children, 13 wakiwa wana umri wa chini ya mwaka mmoja.

Mtoto mmoja alizaliwa hatatimiza hata miezi miwili.

Haki miliki ya picha
UNHCR

Image caption

Miongoni mwao ni watoto 65 children, 13 wakiwa wana umri wa chini ya mwaka mmoja

Watu wengi wenye matumaini ya kupata fursa ya kwenda Ulaya huishia nchini Libya ambako hushikiliwa kwenye vituo vya mahabusu katika hali mbaya.

Hali imekuwa mbaya zaidi kutokana na kuimarika kwa mapigano yanayoendelea kwenye maeneo yanayouzingira mji mkuu Tripoli.

Haki miliki ya picha
UNHCR

Takriban watu 600 wamepoteza maisha yao katika makabiliano ya hivi karibuni nchini Libya, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Wiki iliyopita, madereva wawili wa magari ya kubebea wagonjwa walikufa baada ya kupigwa risasi walipokuwa katika eneo la mashambulizi kuwaokoa waathiriwa . UNHCR imerejea tena wito wake kwamba lkuwalenga raia na wafanyakazi wa huduam za kibinadamu ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa , na limetoa wito wahusika wawajibishwe.

Haki miliki ya picha
UNHCR

Image caption

Uokoaji wa kibinadamu unahitajika zaidi nchini Libya ,” amesema Jean-Paul Cavalieri, mkuu wa UNHCR nchini Libya.

“Uokoaji wa kibinadamu unahitajika zaidi ,” amesema Jean-Paul Cavalieri, mkuu wa UNHCR nchini Libya.

“Ni muhimu kuwaokoa wakimbizi ambao njia yao tu ya kuepuka mateso ni kuweka maisha yao mikononi mwa wafanyabiashara haramu ya watu na wanaowasafirisha kwa njia haramu katika bahari ya Mediterranean.”

Huku vita vya Libya vikishamiri na kiutishia maisha ya wahamiaji, UNHCR inatoa wito tena kwa mataifa kujitokeza haraka na kutoa misaada ya kibinadmau na kuwaondosha wahamiaji ili kuwapatia usalama wakimbizi wanaoishi katika mahabusu nchini LibyaSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *