Agnes Tirop: "Alikuwa mnyenyekevu, mwenye malengo na kutabasamu"


th

Chanzo cha picha, Getty Images

Risala za rambi rambi zimekuwa zikimiminika baada ya kifo cha Agnes Tirop wa Kenya, ambaye alikutwa amekufa siku ya Jumatano, na nahodha wake wa zamani wa riadha Julius Yego akiwa miongoni mwa wanaoongoz katika kutoa risala hizo .

Tirop mwenye umri wa miaka 25 alikutwa ameuawa kwa kuchomwa kisu nyumbani kwake, na polisi wamemtaja mumewe kuwa mshukiwa .

Wakati Tirop, ambaye alimaliza wa nne katika fainali ya mwaka huu ya Olimpiki ya mbio za mita 5000 na kushinda medali ya shaba katika mbio za mita 10,000 kwenye Mashindano ya Dunia ya Riadha ya 2019, Yego alikuwa nahodha wa timu yake.

“Alikuwa msichana mchanga wa kipekee ambaye alikuwa akifanya kazi kwa bidii kuwa mmoja wa wanariadha wakuu ulimwenguni,” Yego aliambia kipindi cha Newsday cha BBC World Service.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *