Agnes Tirop:Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta awaagiza polisi kuchunguza mauaji ya mwanariadha wa olimpiki


TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Agnes Tirop wa Kenya alivunja rekodi ya ulimwengu ya mbio za kilomita 10 za wanawake huko Ujerumani mnamo Septemba

Rais Uhuru Kenyatta amejiunga na tasnia ya riadha nchini Kenya katika kumuomboleza Mwanariadha wa Olimpiki Agnes Jebet Tirop ambaye alikutwa amekufa nyumbani kwake katika mji wa Iten, Kaunti ya Elgeyo Marakwet Jumatano.

Agnes Tirop, mwenye umri wa miaka 25, alikuwa katika kikosi cha wanamichzo wa Kenya walioshinda mashindano ya Olimpiki ya Tokyo ya mwaka 2020 ambayo yalicheleweshwa ambapo aliiwakilisha nchi katika mbio za mita 5,000 na kumaliza katika nafasi ya 4 kwenye fainali.

Katika ujumbe kuifariki familia, marafiki, jamaa, na wadau katika mchezo wa riadha, Rais alimumboleza Agnes kama shujaa na bingwa wa Kenya ambaye kifo chake ni pigo kubwa kwa matamanio ya michezo na hadhi ya nchi.

Chanzo cha picha, Getty Images

“Inasikitisha, ni bahati mbaya kabisa na na jambo la huzuni kwamba tumepoteza mwanariadha mchanga na aliyeiletea nchi fahari akiwa na umri mdogo wa miaka 25, kupitia ushujaa wake katika riadha ya ulimwengu ikiwa ni pamoja na katika mashindano ya Olimpiki mwaka huu ya Tokyo ambapo alikuwa sehemu ya timu ya Kenya huko Japan, “Rais alisemaSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *