Ahmaud Arbery: Wazungu watatu wapatikana na hatia ya mauaji ya mtu mweusi aliyekuwa mazoezini


Ahmaud Arbery alikuwa na umri wa miaka 25 alipouawa

Chanzo cha picha, Family photo

Maelezo ya picha,

Ahmaud Arbery alikuwa na umri wa miaka 25 alipouawa

Wanaume watatu wamepatikana na hatia ya kumuua mtu mweusi aliyekuwa akijfanya mazoezi kukimbia mwaka jana katika kesi ambayo iligeuka kuwa kilio cha kudai haki ya rangi ya waandamanaji.

Ahmaud Arbery, mwenye umri wa miaka 25 alipigwa risasi na kuuawa Februari 2020 katika makabiliano na Travis na Gregory McMichael na jirani wake, William Bryan.

Wanaume hao walijitetea kwa kusema kuwa walichukua hatua ya kumpiga risasi katika kujilinda , lakini waendesha mashitaka walisema rangi ilikuwa ni sababu ya kumpiga risasa.

Wanaume hao sasa wanakabiliwa na hukumu za kifungo cha maisha jela.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *