Apple yaondoa app ya Quran China Kwa nini


Someone reading the Koran on a smartphone

Chanzo cha picha, Getty Images

Apple imefuta moja ya program tumishi maarufu ya Quran duniani kutoka kwa mtandao wake nchini China. Kampuni hiyo imechukua hatua hiyo kufuatia ombi kutoka kwa maafisa wa China.

App ya Quran Majeed inapatikana kote duniani kupitia Apple Store. Karibu watu 150,000 walishirikisha maoni yao kupitia njia ya maoni. App hiyo pia inatumiwa na mamilioni ya waumini wa Kiislam duniani.

BBC inafahamu kuwa app hiyo iliondolewa baada ya kushirikisha maudhui ya ambayo yanaenda kinyume na sheria.

Serikali ya China haijatoa tamko lolote kuhusiana na hatua hiyo licha ya ombi la BBC la kupata kauli yao.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *