Ballon d'Or: Wajue wachezaji watano wa Afrika waliokaribia kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa soka duniani


q

Chanzo cha picha, Getty Images

Miaka miwili baada ya tuzo ya Ballon d’Or kutolewa kwa Lionel Messi, sherehe za tuzo hizi zinarejea tena mwaka huu kumtambua mchezaji aliyefanya vizuri zaidi mwaka huu. Tuzo hizi zinafanyika mwaka huu baada ya kuahirishwa mwaka 2020 kutokana na janga la Corona na tayari orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo hiyo ya juu kabisa mwaka huu inayotolewa kwa mchezaji binafsi imeshawekwa wazi.

Waafrika wawili Mohamed Salah kutoka Misri anayechezea klabu ya Liverpool na Riyad Mahrez kutoka Algeria anayechezea Manchester City ni miongoni mwa wachezaji 30 wanaowania tuzo hiyo.

Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo mwaka 1956, ni mwafrika mmoja tu George Weah ambaye sasa ni rais wa Liberia, aliyewahi kutwaa tuzo hiyo, mwaka 1995. Lakini wapo wachezaji kadhaa wa Afrika waliokaribia kabisa kuibeba tuzo hiyo, lakini pengine uwepo wa Lionel Messi (Argentina) anayekipigia PSG aliyetwaa mara 6 na Cristiano Ronaldo (Ureno) wa Manchester United aliyetwaa mara 5 umepunguza fursa kwa waafrika wengi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

George Weah (kulia) akikabidhi tuzo yake ya Ballon d’Or aliyoitwaa mwaka 1995 wakati huyo akiichezea AC Milan kwa Rais wa Liberia wakati huo, Ellen Johnson Sirleaf. Ilikuwa June, 2013 kwenye mchezo maalumu wa amani. Weah ni Rais wa sasa wa Liberia na muafrika pekee kutwaa Ballon d’Or.

Nyota hawa wawili katika kipindi cha muongo mmoja uliopita wamekuwa watawala wa soka, wakibadilishana hii tuzo wao wawili. Katika miaka 14 iliyopita tangu 2008 ni mwaka 2019 pekee alitwaa Luka Modric wa Croatia na klabu ya Real Madrid, huku mwaka jana haikufanyika, lakini miaka mingine yote wamekuwa wakibadilishana.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *