Benki ya dunia yaunga mkono hatua ya serikali ya Tanzania kuwarejesha wasichana shuleni


Waziri wa elimu Tanzania, Joyce Ndalichako

Chanzo cha picha, DAILYNEWS

Benki ya Dunia imeunga mkono tangazo la Serikali ya Tanzania la kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa elimu, vikiwemo vile ambavyo vimewazuia wasichana wajawazito au kina mama wachanga kuhudhuria shule katika mfumo rasmi.

Uamuzi huu muhimu unasisitiza dhamira ya nchi ya kusaidia wasichana na wanawake vijana na kuboresha nafasi zao za kupata elimu bora, ilisema taarifa ya benki hiyo

Benki ya dunia imesema zaidi ya wasichana 120,000 huacha shule kila mwaka nchini Tanzania. 6,500 kati yao kwa sababu ni wajawazito au wana watoto.

”Benki ya Dunia inaunga mkono kwa dhati sera zinazohimiza elimu ya wasichana na zinazowezesha wanafunzi wote kusalia shuleni.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *