Biden na Putin wakutana GenevaMaafisa wa Marekani na Russia wanasema mazungumzo yao yatadumu kati ya saa nne mpaka tano.

Viongozi hao wamekubaliana kukutana katika kikao cha ana kwa ana wakiwa pamoja na mawaziri wao wa mambo ya nje, Antony Blinken upande wa Marekani na Sergei Lavrov wa Russia.

Taarifa za pande mbili zinaeleza kuwa mazungumzo ya baadaye yatashirikisha kundi jingine pana.

Balozi wa Marekani huko Russia John Sullivan na yule wa Russia hapa Marekani Anatoly Antonov ambao walirudi katika nchi zao mapema mwaka 2021 kufuatia uhusiano mbaya kati ya nchi hizo mbili wanatarajiwa kushiriki mkutano huo mjini Geneva.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *