Burundi yatangaza kuwa na wagonjwa wa corona kwa mara ya kwanza


HABARI ZA HIVI PUNDE

Burundi yathibitisha kuwa na wagonjwa wawili wa corona.

Waziri wa afya nchini humo ametangaza watu wawili ambao ni raia wa Burundi kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Raia hao ambao wote ni wanaume, mmoja ana umri wa miaka 56 huku mwingine ana umri wa miaka 42, na walikuwa wanawasili kutoka Rwanda na Dubai, Waziri alisema.

Naye msemaji wa rais wa Burundi, bwana Jean Claude Karerwa ameiambia BBC kuwa Mungu atawalinda na maambukizi haya kwa sabbu Mungu ameiweka serikali ya Burundi ka tika sehemu ya kipekee.

Taifa la Burundi linatarariwa kuwa na uchaguzi mkuu wa rais tarehe 20 Mei.

Bwana Karerwa alisema kuwa uchaguzi unaweza kuwa na mabadiliko kama tu maambukizi hayo ya Covid 19 yatazidi nchini humo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *