Chama cha Wauguzi chaikosoa CDC kwa tamko la kutokuvaa barakoaMkurugenzi mtendaji wa Umoja wa Kitaifa wa Wauguzi, Bonnie Castillo amesema huu muongozo mpya wa CDC haulingani na sayansi, na haulindi afya ya umma na kutishia maisha ya wagonjwa.

Pia amesema muongozo huu haulindi maisha ya wauguzi na wafanyakazi wengine wa mstari wa mbele kote nchini na kuongezea huu si wakati wa kulegeza masharti ya kujilinda.

Mkurugenzi huyo alionyesha hasira juu ya hatua hiyo ya CDC, akihoji vipi wanafanya maamuzi kama hayo wakati bado Marekani ipo katikati ya janga baya sana kuwahi kutokea.

Rais wa umoja huo Jean Ross amesema kama CDC imetambua vyema sayansi ya jinsi virusi hivi vinavyoambukiza, huu muongozo mpya kamwe usingetolewa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *