Champions League: Ajax yawika dhidi ya Tottenham ugenini


Wachezaji wa wa pande pinzani wakikabiliana

Haki miliki ya picha
Getty Images

Tottenham italazimika kubadili matokeo yake dhidi ya Ajax ili kuweza kutinga nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya baada ya kupoteza nyumbani katika awamu ya kwanza ya nusu fainali.

Klabu hiyo ya Uholanzi ilijipatia goli la ugenini wakati Donny van de Beek alipochukua pasi ya Hakim Ziyech na kumfunga kipa wa Spurs Hugo Lloris.

Fernando Llorente na Toby Alderwiredld wote walipoteza nafasi nzuri wakiwa peke yao.

David Neres wa Ajax karibu afunge goili la pili baada ya shambulio lake kugonga chuma cha goli.

Tottenham hawajawahi kutinga fainali ya vilabu bingwa ama hata ile ya Yuropa na watalazimika kufunga katika awamu ya pili ya nusu fainali mjini Amstadam siku ya Jumatano ijayo ili kuweza kuwa na fursa ya kusonga mbele.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Spurs huenda ikakosa huduma za beki Jan Vertonghen katika mechi hiyo baada ya kuvunjika pua yake alipogongana na mchezaji mwenza Alderweireld pamoja na kipa Ajax goalkeeper Andre Onana.

Vertonghen ambaye pia alionekana kuumia aliruhusiwa kurudi uwanjani kabla ya kusaidiwa kutoka nje na maafisa wa afya wa Spurs.

Washindi wa mechi hiyo watakutana na Barcelona au Liverpool katika mechi ya fainali itakayochezwa mjini Madrid mnamo Juni mosi.

Ajax ilionyesha mchezo ulio pevuka

Haki miliki ya picha
Getty Images

Hatua ya Ajax kutinga nusu fainali kumeifanya kuwa ndio timu inayojadiliwa sana barani Ulaya baada ya kuiadhibu na kuwaondoa katika kinyanganyiro hicho bingwa mtetezi Real Madrid pamoja na mabingwa wa Itali Juventus.

Na ilikuwa rahisi kuona ni kwa nini timu hiyo ndio inayozungumzwa sana baada ya kuonyesha mchezo wa hali ya juu ugenini.

Ajax ndio ilioanza kutawala mchuano huo kabla ya kupata bao hilo muhimu na baadaye ikazuia presha zote za Tottenham ili kuibuka mshindi.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Nahodha Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 19, alionyesha uongozi wa zaidi ya miaka yake katika safu ya ulinzi , akiwandaa na kuwaagiza mabeki wenye uzoefu mkubwa na utaalam.

Frenkie de Jong ,21, ambaye anaelekea Barcelona walishiriikiana na kiungo wa kati mwenza Van de Beek, ambaye ni mkubwa wake kwa mwaka mmoja , hiki ni kikosi cha Ajax chenye umahiri na ujana ndani yake ambao wanacheza kulingana na utamaduni wa klabu hiyo.

Ajax hawakupigiwa upatu kufika nusu fainali lakini hii ni timu ambayo inaonekana kuwa na motisha na uwezo wa kushinda ubingwa huu.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *