COP26: Ni kitu gani, kwanini muhimu, na nini tutarajie?


Illustration showing a person trying to put out fire that has engulfed planet Earth.

Chanzo cha picha, Getty Images/BBC

COP26 unafanyika nchini Scotland mwaka huu na matarajio ya tukio hili yanazidi kuwa makubwa. Lakini mkutano huu wa mabadiliko ya tabia nchi una nini hasa?. Kwa makala haya itakusaidia kufahamu masuala muhimu kuhusu mijadala mingi ya mabadiliko ya tabia nchi.

COP26 ni nini?

COP – ni kifupi cha maneno ya kiingereza (Conference of the Parties) – ukiwa ni mkutano wa mwaka ukiyaleta pamoja mataifa 197 duniani kuzungumzia kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na namna gani nchi hizo na watu wote wamejipanga kukabiliana na mabadiliko hayo.

Ni sehemu ya maazimio ya umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi – ni mkataba wa kimataifa uliotiwa saini na karibu kila nchi ulimwenguni unaokusudia kupunguza athari za shughuli za kibinadamu kwenye masuala ya hali ya hewa.

COP26 utakuwa mkutano wa 26 tangu makubaliano ama mkataba huo uanze kutekelezwa Machi 21 mwaka 1994. Mwaka huu utafanyika nchini Scotland katika jiji kubwa la Scotland, Glasgow, kati ya Novemba 1-12.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *