Coronavirus: Jinsi marufuku ya kutoka nje ya virusi vya corona inavyowaathiri wanawake kwa kunyanyaswa


Man standing ominously over a woman.

Haki miliki ya picha
James Mobbs/BBC

Image caption

Visa vya unyanyasaji wa kijinsia ndani ya ndoa vimeripotiwa kuongezeka katika nchi za Marekani, Ufaransa na Australia katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women) Phumzile Mlambo-Ngcuka ameiambia BBC kuwa tofauti na Marekani na Uingereza , ambako vituo vya vya unyanyasaji wa wanawake vimepokea ongezeko la visa hivyo, hali huenda ikawa ni kinyume katika mataifa yanayoendelea.

“Haiwezekani kwa wanawake kutoka nchi zenye uchumi wa wa chini, katika mataifa kadhaa, kuripoti visa vya unyanyasaji wa nyumbani wakati wanaishi katika nyumba zenye chumba kimoja au viwili na wanaowanyanyasa”anasema Bi Mlambo-Ngcuka.

“Tunatarajia kushuhudia kupungua kwa ripoti za aina hii ya unyanyasaji nyakati za amri za kutotoka nje na ukimya huo ni wa kutia hofu hata zaidi. Ilikua ni kadhaa tu baada ya mlipuko mbaya zaidi wa Ebola katika mataifa ya Afrika Magharibi ambapo tuligundua ongezeko la unyanyasaji wa kijinsia majumbani .”

BBC imezungumza na wanawake wawili katika nchi za India na Marekani, ambao kwa sasa wako katika marufuku ya kutotoka nje na wanaishi na wanaume wanaowanyanyasa. Hizi ni simulizi zao.

Haki miliki ya picha
James Mobbs/BBC

Image caption

Kipato cha familia ya Geeta kimeporomoka mara tatu toka ulipoingia mlipuko wa virusi vya corona.

Geeta, 27, India

Mahojiano haya yalifanyika siku moja kabla India itangaze sheria ya kutotoka nje kabisa kwa muda wa siku 21 ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Geeta anaamka saa kumi na moja alfajiri, mumewe amejilaza kando yake. Anakoroma kwa nguvu.

Usiku uliopita alikua amerudi nyumbani akiwa amelewa na mwenye hasira.

Mlipuko wa coronavirus unamaanisha kuwa ni watu wachache tu wanaotumia usafiri wa umma, kwahivyo kama dereva wa Bajaji (tuk tuk) pato la Vijay limeshukwa kutoka rupia 1500 kwa siku (takriban dola 20), hadi rupia 700 ( dola 9 na nusu), kwa wiki hiyo (kabla ya marufuku ya kutoka nje).

“Mambo yatakuwa namna hii kwa siku ngapi?” alipaza sauti, huku akitupa chupa za pombe kali kwenye ukuta. Watoto wanne wa Geeta, mkubwa akiwa na umri wa miaka saba na wadogo zake watatu walikua wamejificha nyuma yake kwa hofu.

Hatimae baada ya kelele mume wake Vijay alikwenda kulala kwenye godoro dogo ambalo hulalia na familia nzima.

“Ilichukua muda kuwatuliza watoto,” anasema Geeta, “Wamemuona baba yao akiwa mwenye hasira mara nyingi katika maisha yao, lakini wiki iliyopita hali yake imekuwa mbaya sana. Wamemuona akirusha vitu ukutani na kunivutavuta nywele.”

Her husband would leave at around 7am, returning for lunch and a nap, leaving again after the two older children returned from school.

Nyumba ya chumba kimoja

Geeta ana umri wa miaka 27 na ameolewa kwa muda wa miaka 12. Ameolewa na mwanaume anayemzidi miaka 11, amempiga mara nyingi kuliko anavyoweza kukumbuka, mara ya kwanza ikiwa ni usiku wa harusi yao.

Alijaribu kuachana naye mara moja, lakini hakumruhusu achukue watoto wake.

Geeta na familia yake wanaishi katika nyumba ya chumba kimoja, katika eneo la watu wenye kipato cha chini linaloitwa mohalla, katika maeneo ya vijijini ya Rajasthan.

Kwa siku ya kawida Geeta hutembea kilomita moja kuteka maji ya kutumia kwa ajili ya siku hiyo moja. Baada ya kuyafikisha nyumbani, husubiri nje huku akipiga gumzo na wanawake majirani zake huku akimsubiri muuza mboga awasili na kikapu cha mboga. Baada yakununua mboga za siku, Geeta huanza kuandaa kifungua kinywa.

Mume wake huondaka majira ya saa moja asubuhi, na kurejea kwa ajili ya chakula cha mchana na kisha hujilaza kwa usingizi wa muda mfupi , halafu huondoka tena baada ya watoto wawili wakubwa kurejea Kutoka shuleni.

Darasa la siri

“Lakini mambo yalibadilika wakati shule ilipofungwa tarehe 14, Machi,” anasema, “Halafu watoto wakawa nyumbani wakati wote na wakaanza kumkera mume wangu.”

“Kwa kawaida huwa anamalizia hasira kwangu, lakini sasa ameanza kuwafokea kwa mambo madogo kama vile wanapoacha kikombe sakafuni. Halafu ninaanza kusema kitu fulani kumsahaulisha ili anikasirikie mimi badala ya watoto, lakini kadri tunavyoendelea kuwa pamoja ninapungukiwa na la kumwambia ili kuzima hasira yake.”

Geeta alikua na mpango. Wakati mume wake alipokua kazini na baada ya kusafisha nyumba, alikua akitembea na kwenda hadi katika ofisi moja iliyopo karibu.

Pale alikuwa akihudhuria masono ya siri yaliyokua yameandaliwa na jamii ambako wanawake kama yeye walikua wakijifunza ushonaji, kusoma na kuandika.

Geeta anataka kupata ujuzi wa kutosha ili wakati atakapofikia umri wa miaka 30 awe ana uwezo wa kujitegemea kifedha na kuondoka na watoto wake.

Darasani, Geeta pia hukutana na washauri nasaha ambao wamepata mafunzo ya kuwasaidia waathiriwa unyanyasaji wa majumbani.

Wanandoa wanyanyasaji

Siku 21 za marufuku ya kutotoka nje nchini India , iliyoanza tarehe 24 Machi, imezuia hili. Madarasa yamesimamishwa na haiwezekani kwa washauri wa kijamii kuwatembelea wanawake walio katika hali za kunyanyaswa.

Vimlesh Solanki, afisa wa kujitolea katika taasisi ya Sambhali Trust inayowasaidia wanawake katika Jodhpur, mji wa pili kwa ukubwa katika Rajasthan, anasema coronavirus imewaweka wanawake hatarini.

“Kutotoka nje kabisa kila siku inamaanisha kusumbuliwa kabisa. Kwa sasa hakuna maduka madogo ya bidhaa ya mtaani kwa hiyo kila siku wanahitaji kusafiri mbali kwenye maduka ya jumla.

Hali zinazokanganya kama hizi zinanasababisha vitu vingi vinavyowakera wame zao ambao tayari ni wanynyasaji.”

Haki miliki ya picha
James Mobbs/BBC

Kai, 19, New York

Kai aliacha kuzungumza kwenye simu yake na kuanza kuandika taratibu.

“Mama anataka mimi nikae na wewe .”

Akautuma ujumbe.

Jibu likaja haraka “hiyo ni sawa.”

Halafu Alhamisi iliyopita Kai mwenye umri wa miaka, 19, akarejea katika nyumba ambayo wakati mmoja aliapa kutorejea tena.

“Siku alipoingia tena kwa mara ya pili katika nyumba ile ubongo wangu uliacha kufanya kazi,” alisema kwa upole, “Kila kitu kilizima, kila hisia.”

Alirejea tena kwa baba yake, mwanaume ambaye alimyanyasa kimwili na kingono kwa miaka mingi.

Huwezi kusikiliza tena

Coronavirus: Kufungiwa ndani na anayeninyanyasa

Wiki mbili zilizopita Kai alidhani coronavirus kilikua ni kitu ambacho kingebadili mambo. Halafu mambo yakabadilika.

Wafanyakazi katika duka ambako mama yake alikua akifanyia kazi walikuwa hawana amani. Taarifa za kuongezeka zaidi kwa maambukizi ya virusi vya corona zimesambaa, na virusi vilikuwa vimeenea katika zaidi ya nchi 170 sasa vimefika katika maeneo ya jiji lao la New York, iliwatia hofu watu.

Kufanya kazi katika duka ilimaanisha kuwa kuchangamana na wateja kila siku, na hakuna anayejua kuwa baadhi yao wanaweza kuwa na virusi vya corona .

Kupoteza kazi

Mama yake Kai na wafanyakazi wenzake walikua na hofu juu ya kuchangamana na wateja, lakini hawakupaswa kuendelea kuwa na uoga kwa muda mrefu. Duka lilitangaza kuwa linafungwa kwa muda na wafanyakazi watalazimika kuachishwa kazi.

Mama yake Kai alipoteza pato lake la (walau dola 15 kwa saa) na akaambiwa atakua na bima ya afya kwa siku tano pekee.

Nyumba ilikua tayari imejaa. Kai, mama yake na dada yake waliishi katika nyumba ya vyumba vitatu, na watu wengine wawili.

Hali ilianza kumuelemea mama yake Kai, ambaye alikua na matatizo ya afya ya akili katika kipindi chote cha maisha ya Kai.

“Halafu Alhamisi iliyopita alikua na tatizo anamsema Kai, “Alipiga kelele ‘mambo ni ya mabaya hapa, unapaswa kwenda katika nyumba ya baba yako’.”

Maneno hayo ya mama yake yalimtia hofu kubwa Kai. Akajificha katika chumba chake, akitumai kuwa kama atampatia mama yake muda wa kufikiria atabadili uamuzi wake.

Lakini wakati Kai aliporudi sebuleni mama yake , “Ni kwanini bado upo hapa?”

Ilikua ni miezi michache tu baada ya Kai kuanza matibabu kwa ajili ya miaka kadhaa ya unyanyasaji wa kingono alioupitia alipomtembelea baba yake – ambaye alikua ametengene na mama yakealipokua mtoto mdogo.

Imemchukua miaka mingi ya kufikiria kupata usaidizi wa kitaalamu.

Bado hajaweza kumwambia mama yake na dada yake unyanyasaji wa kingono aliofanyiwa na baba yake. Unyanyasaji huo umemfanya pia ajitenge na marafiki zake .

Unyanyasaji wa Kingono

Unyanyasaji wa kimwili ulifanyika dhidi yake wakati tu Kai alipofanya kitu kilichomkera baba yake.

Kwa hiyo mpango wa Kai ulikua ni kuwa mbali na yeye.

Aliondoka chumbani kwake tu alipokua akikimbilia bafuni na wakati alipokwenda jikoni kujipikia chakula.

Lakini hapakua na sababu ya unyanyasaji wa kingono. Unyanyasaji huo ulitegemea kile baba yake alichokiona kwenye mtandao.

Wakati wa mwisho walipokama pamoja ni wakati wa kimbunga Sandy mwaka 2012.

Wakati walipokosa umeme nyumbani kwao, unyanyasaji ulikua ni mbaya sana.

Hadi sasa hakuna kilichotokea.

‘Matarajio yananiua’

“Alijifanya kana kwamba tunaishi katika wakati wa ajabu kuwahi kushuhudiwa katika historia, lakini hazungumzii kuhusu unyanyasaji ,”anasema, “Hilo linanifanya nijihisi kama mwendawazimu. Hajafanya lolote bado lakini matarajio yangu ya kwamba atazungumzia unyanyasaji alionifanyia yananiua.”

Kai hutumia muda wake siku nzima kwenye mtandao. Hivi karibuni amekua akitazama video za makala katika YouTube video kuhusu filamu . Anafurahia kutazama uchanganuzi wa filamu.

Ingekua ni coronavirus, Kai angejaribu kutafuta mahala pa kuishikuliko kuishi na baba yake , lakini anahofia kwamba kuishi mahala padogo kunaweza kuongeza fursa ya kusambaa kwa virus.

Bado yuko katika wakati wa kuficha unyanyasaji wake na hata hawezi kufikiria kumshitaki baba yake polisi.

Anatumai mama yake atamruhusu kurejea kwake tena haraka au mlipuko wa coronavirus outbreak utakwisha na aweze kutafuta mahali kwingine pa kuishi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *