Coronavirus: Kwa nini virusi vya corona husambaa haraka miongoni mwa wanadamu


coronavirus

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Wataalam wanakubaliana kwamba virusi kama SARS havijawahi kuonekana

Ni kifurushi kidogo cha nyenzo za jeni iliozungukwa na protini na ukubwa wake ni moja ya elfu ya unywele wa binadamu.

Hata hivyo, virusi hivi hatari kwa jina SARS-CoV-2, tayari vimesambaa katika kila nchi duniani na vimeambukiza zaidi ya nusu milioni ya watu tangu vilipotambulika nchini China mwezi Disemba 2019.

Virusi kama hivi, kutoka familia ya coronavirus pia vinaweza kusababisha maradhi kwa wanyama.

Ni virusi saba vinavyojulikana ikiwemo SARS-CoV-2, ambavyo vimesambaa kutoka kwa wanyama na kuingia kwa binadamu.

Na ndio maana vimehusishwa na milipuko wa magonjwa hatari zaidi katika historia mwaka 1918, 1957, na milipuko ya Influenza pamoja na SARS, MERS na Ebola .

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mataifa kadhaa yamelazimika kuweka vito vipya ili kuwahudumia wagonjwa wa covid -19

Lakini wataalamu wanakubaliana kwamba kirusi hatari kinachosambaa haraka kama hiki cha corona hakijawahi kuonekana.

Hivyo basi tunauliza ni nini haswa kinachofanya virusi vya SARS-CoV-2 kushambulia seli za mwanadamu na kusambaa kwa haraka?

Jinsi vinavyoingia katika seli ya binadamu

Tafiti kadhaa zinachunguza ni taratibu gani za kibaiolojia virusi hivyo vinatumia ili kuambukiza seli za wanadamu.

Baadhi ya wanasayansi wanaangazia kile kinchoitwa Miba, ambapo miba hiyo yenye umbo la protini hujitokeza katika sakafu yake na kutengeza corona.

Tafiti nyingine zinachunguza njia inayotumika na virusi hivyo ndani ya mwili wa mwanadamu.

Haki miliki ya picha
Getty

Image caption

lengo la virusi hivyo vinapoingia katika seli ya mwili wa bindamu ni kuzaana

Coronavirus ina jina hilo kwa sababu hutokana na protini yenye mwiba inayojitokeza kutoka katika sakafu yake na miba hiyo ndio inayosaidia virusi hivyo kuingia katika seli kulingana na Panagis Galiatsatos, Profesa wa magonjwa ya mapafu na wagonjwa mahututi kutoka chuo kikuu cha tiba cha Johns Hopkins University.

Lengo la virusi hivyo punde vinapoingia mwilini ni kuzaana na ili kufanikiwa kufanya hivyo ni sharti viingie katika seli.

”Virusi vinavyosababishwa na homa ya kawaida, SARS ya 2003 na MERS vyote vina miba , na kile kinachobaini jinsi vitakavyoingia katika seli ni aina ya receptor itakayotumika” , anaelezea mtaalam.

Baadhi ya wanafunzi wamefanikiwa kuonyesha kwamba SARS-CoV-2 hujiondoa katika receptor – ama protini kwa jina ACE2 .

Protini hii hupatikana katika maeneo mengi ya mwili wa mwanadamu kama vile mapafu, moyo, figo na matumbo na kazi yake kuu ni kupunguza shinikizo la damu.

“ACE2 ipo katika sakafu ya seli na wakati virusi hivyo vinapoitambua, vinashikana na hivyobasi kuingia katika seli , kulingana na Sarah Gilbert, profesa wa chanjo katika chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza .

Haki miliki ya picha
Getty

Image caption

Kikohozi kinachotokea wakati mapafu yanapojaribu kukabiliana na maambukizi

Punde tu vinapoingia ndani , vinatumia seli hiyo kama kiwanda cha kuzalisha virus zaidi .

Baadaye kinatoroka katika seli ambapo kinawacha ganda moja la kirusi kinachoendelea kuambukiza seli nyengine.

Virusi vya mapafu , kama vile mafua , hupenda sana kuzaana puani na kwenye koo ambapo vinaweza kusambazwa rahisi kupitia kikohozi na kupiga chafya.

Lakini kuna virusi vingine ambavyo huzaana katika eneo la chini la mapafu , ambapo husambaa kwa urahisi lakini huwa hatari zaidi.

Kipengele muhimu

SARS-CoV-2, hatahivyo vina tabia tofauti. Hupatikana katika mapafu ya juu na yale ya chini , vikisambaa kupitia kikohozi na mapafu ya chini na kusababisha magonjwa ya mapafu ambayo yanaweza kuwa hatari zaidi.

Haki miliki ya picha
Getty

Image caption

Virusi vya SARS-CoV-2 hupatikana juu na chini ya mapafu

ACE2 ni nyingi mwilini na hupatikana katika viungo vingi vya mwili wa mwanadamu, kulingana na profesa Galiatsatos.

Ni katika seli za mdomo, koo, figo moyo na hata utumbo ambapo baadhi ya wagonjwa huhisi kisunzi na kuharisha.

Lakini cha kutishia ni kwamba virusi hivi pia viko katika alveoli sehemu nyepesi za hewa kwenye mapafu ambapo uhamishaji wa gesi hufanyika. ”

Wakati virusi hivyo vinapoharibu seli kulingana na mtaalamu huyo kunakuwepo baadhi ya dalili zinazopatikana katika mtu aliyeambukizwa na covid-19 kama vile tatizo la kupumua, kikohozi ambacho hutokea wakati mapafu yanajaribu kukabiliana na maambukizi.

Dalili na maambukizi

Mojawapo ya tofauti kati ya SARS-CoV-2 na viruis vya corona kama vile SARS ya 2003 ama MERS , ni kwamba virusi hivi huzaana kwa haraka.

Hatua hiyo husababisha dalili za ugonjwa huo kuonekana haraka na kwamba mgonjwa anaweza kujitenga kwa haraka bila kusababisha maambulkizi zaidi.

Katika virusi vya covid 19 , dalili hazionekani haraka na watu wanaweza kupata maambukizi yake na kuusambaza bila kuonyesha dalili za ugonjwa huo.

“SARS (2003) vilikuwa virusi vilivyozaana katika mapafu na kuambukizwa kwa urahisi kwa sababu dalili zake zilionekana kwa haraka na mgonjwa aliweza kujitenga kwa haraka kulingana na profesa David Hymann, mtaalamu wa magonjwa ya maambukizi ambaye aliongoza ujumbe wa WHO wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo.

Lakini virusi vyote vyote viko tofauti , na virusi hivi vipya vinaonekana kuwa na uwezo wa kusambaa kwa haraka na kwa urahisi miongoni mwa bindamu.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Virusi vipya vya corona husambaa kwa urahisi

”Tunaamini kwamba mtu anaweza kuanza kumuambukiza mtu mwengine kabla ya dalili kuonekana , siku moja kabla , na baadaye kuendelea kuambukiza kwa takriban siku saba”, anaongezea.

Hapa ndiposa hatari kubwa ya SARS -CoV-2 huonekana na hivyobasi ndio sababu serikali nyingi zinasisitiza kuhusu kukaa mbali. Virusi hivyo vinaweza kuishi iwapo vitapata mtu mwengine wa kuambukiza .

Wakati mtu anaposalia nyumbani kwa siku 14 inapunguza fursa ya kuambukiza mtu mwengine.

”Kwa sasa hiyo ndio njia pekee inayoweza kutumika . Juhudi zinafanywa kutafuta chanjo ama tiba , lakini hatua zilizopigwa kisayansi sio za haraka kama vile tunavyohitaji na kila kitu kitachukua muda”, alisema Panagis Galiatsatos.

Katika kitabu cha Art of War “Sun Tzu anasema kwa wewe kuweza kushinda vita ni sharti umjue adui yako . lakini unapotambua kwamba adui yako ni mjanja unalazimika kuwa mvumilivu . Ni hicho ndicho naweza kusema kuhusu virusi hivi.

Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.

Visa Vifo
Marekani 164,371 3,162
Italia 101,739 11,591
Uhispania 87,956 7,716
Uchina 82,240 3,309
Ujerumani 66,885 645
France 44,550 3,024
Iran 41,495 2,757
Uingereza 22,141 1,408
Uswizi 15,922 359
Belgium 11,899 513
Netherlands 11,750 864
Uturuki 10,827 168
Korea Kusini 9,786 162
Austria 9,618 108
Canada 7,448 89
Ureno 6,408 140
Israel 4,695 16
Brazil 4,661 165
Australia 4,516 18
Norway 4,462 32
Sweden 4,028 146
Jamuhuri ya Czech 3,001 23
Ireland 2,910 54
Malaysia 2,626 37
Denmark 2,577 77
Chile 2,449 8
Romania 2,109 65
Poland 2,055 31
Luxembourg 1,988 22
Ecuador 1,966 62
Japan 1,953 56
Urusi 1,836 9
Kashmir inayotawaliwa na Pakistan 1,717 21
Ufilipino 1,546 78
Thailand 1,524 9
Saudi Arabia 1,453 8
Indonesia 1,414 122
Finland 1,352 13
Afrika Kusini 1,326 3
India 1,251 32
Ugiriki 1,212 46
Mexico 1,094 28
Iceland 1,086 2
Panama 1,075 27
Argentina 966 24
Peru 950 24
Jamuhuri ya Dominica 901 42
Singapore 879 3
Colombia 798 14
Croatia 790 6
Serbia 785 16
Slovenia 756 11
Estonia 715 3
Mili ya Diamond Princess 712 10
Qatar 693 1
Misri 656 41
New Zealand 647 1
Iraq 630 46
Milki za Kiarabu 611 5
Algeria 584 35
Morocco 556 33
Ukrain 548 13
Bahrain 515 4
Lithuania 491 7
Armenia 482 3
Hungary 447 15
Lebanon 446 11
Latvia 376
Andorra 370 8
Bosnia na Herzegovina 368 10
Tunisia 362 9
Bulgeria 359 8
Slovakia 336
Costa Rica 330 2
Kazakhstan 325 1
Uruguay 320 1
Taipei ya China 306 5
Moldova 298 2
Macedonia Kaskazini 285 7
Azerbaijan 273 4
Jordan 268 5
Kuwait 266
Burkina Faso 246 12
San Marino 230 25
Cyprus 230 7
Kisiwa cha Reunion 224
lbania 223 11
Vietnam 204
Oman 179
Puerto Rico 174 7
Cuba 170 4
Afghanistan 170 4
Visiwa vya Faroe 168
Cote d’voire 168 1
Senegal 162
Malta 156
Belarus 152
Ghana 152 5
Uzbekistan 150 2
Honduras 141 7
Cameroon 139 6
Venezuela 135 3
Nigeria 131 2
Mauritius 128 3
Brunei Darussalam 127 1
Sri Lanka 122 2
Maeneo ya Wapalestina 117 1
Cambodia 107
Bolivia 107 6
Guadeloupe 106 4
Georgia 103
Kosovo 94 1
Kyrgystan 94
Martinique 93 1
Montenegro 91 1
Trinidad and Tobago 85 3
Mayotte 82
Jersey 81 2
Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo 81 8
Rwanda 70
Gibraltar 69
Paraguay 65 3
Liechtenstein 62
Guernsey 60
Guam 58 1
Kenya 50 1
Aruba 50
Bangaldesha 49 5
Monaco 49 1
Isle of Man 49
Guiana ya Ufaransa 43
Madagascar 43
Guatemala 36 1
Jamaica 36 1
Polynesia ya Ufaransa 36
Zambia 35
Barbados 34
Uganda 33
El Salvador 32
Togo 30 1
Bermuda 27
Niger 27 3
Mali 25 2
Ethiopia 23
Guinea 22
Congo 19
Tanzania 19
Djibouti 18
Maldivers 17
Saint Martin (Eneo la Ufaransa) 15 1
New Caledonia 15
Eritrea 15
Haiti 15
Bahamas 14
Myanmar 14 1
Dominica 12
Equitorial Guinea 12
Mongolia 12
Visiwa vya Cayman 12 1
Namibia 11
Netherlands Antilles 11 1
Ushelisheli 10
Greenland 10
Syria 10 2
Jamuhuri ya kidemokraia ya watu wa Lao 9
Eswatini 9
Saint Lucia 9
Grenada 9
Suriname 8
Guinea_Bissau 8
Guyana 8 1
Mozambique 8
Libya 8
Angola 7 2
Gabon 7 1
Saint Kitts na Vevis 7
Zimbabwe 7 1
Antigua na Barbuda 7
Mauritania 6 1
Netherlands Antilles 6
Sudan 6 2
Cape Verde 6 1
Benin 6
Vatican 6
Saint Barthélemy 6
Turks nad Visiwa vya Caicos 5
Nepal 5
Chad 5
Fiji 5
Montserrat 5
Nicaragua 4 1
Gambia 4 1
Bhutan 4
Belize 3
Liberia 3
Somalia 3
Botswana 3
Jamuhuri ya Afrika ya Kati 3
Visiwa vya Virgin vya Uingereza 3
Mili ya MS Zaandam 2
Anguilla 2
St St Vincent na Gradines 1
Timor_Leste 1
Papua News Guinea 1
Visiwa vya Virgin vya Marekani


Chanzo: Chuo kikuu cha Johns Hopkins (Baltimore, Marekani), maafisa wa eneoSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *