Coronavirus: Uganda yathibitisha kuwa na wagonjwa 44 wa Covid 19


watoto choir

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Watoto choir

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza visa vipya 11 vya ugonjwa wa Covid-19 nchini humo, wote wakiwa wanakwaya wa kwaya maarufu nchini humo ‘Watoto Children’s Choir.

Kupitia matangazo ya televisheni, alisema kuwa wagonjwa wote wapya walikuwa karantini baada ya kurejea kutoa ughaibuni , ingawa hakueleza afya zao zikoje kwa sasa na walikuwa wametoka taifa gani.

Mara nyingi kwaya hiyo huwa inatumbuiza katika nchi za ughaibuni kama Marekani, Canada na Uingereza.

Mpaka sasa Uganda imethibitisha kuwa na wagonjwa wa Corona 44.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Katika hatua za kukabiliana na maambukizi ya corona, tayari rais wa Uganda Yoweri Museveni ametagaza masharti zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona wiki mbili baada ya kupiga marufuku usafiri wa Umma.

Katika hotuba yake kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni usiku wa Jumatatu Bw. Museveni amepiga marufuku usafiri wa kutumia magari binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku.

Mtu yeyote anayehitaji huduma za dharura za kiafya kama vile kujifungua au kufanyiwa upasuaji anatakiwa kupata idhini kutoka kwa maafisa wa serikali katika ngazi ya Wilaya kabla ya kutoka nyumbani

Wauzaji bidhaa za chakula sokoni watahitajika kuondoka maeneo yao ya biashara hadi pale serikali itakapokamilisha kushughulikia maeneo mapya ya wao kuuzia bidhaa zao .

Rais Museveni pia ameahidi msaada wa chakula kwa watu ambao hawafanyi kazi kutokana na vikwazo vya kukabiliana na covid-19 na hawana uwezo wa kujipatia bidhaa hiyo muhimu.

Bw. Museveni pia ametoa agizo kwa polisi kuwakamata wanasiasa watakaotoa misaada ya chakula kwa jamii na kushtakiwa kwa ”jaribio la mauaji ”

Uganda kufikia sasa imethibitisha kuwa na wagonjwa 33 wa corona na maafisa wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.

Magari binafsi yatazuiwa kuingia barabarani baada ya maelekezo ya awali kutaka magari kubeba abiria watatu pekee kukiukwa, na baadhi ya watu kutumia magari binafsi kuwasafirisha wengine na kuongeza hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo. Limeandika gazeti la New vision la Uganda.

”Isipokuwa kwa ndege za mizigo, malori, magari aina ya pickups na treni, kuanzia siku ya Jumanne tarehe 31 mwezi Machi saa moja, amri ya kutotoka nje itatekelezwa katika nchi yote ya Uganda” Meseveni aliesema.

Alisema kuwa siku 14 zitatumika kubaini na kuwafuatilia na kuwatenga wale wote waliokaribiana na watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Image caption

Usafiri wa umma umepigwa marufuku Uganda

Uganda kwa sasa imethibitisha kuwa na watu 13 walioambukizwa virusi vya corona, hakuna vifo na hakuna aliyepona mpaka sasa.

Kati ya nchi 54 barani Afrika, nchini ya nchi 10 hazijathibitisha kuwa na maambukizi.

Kikosi kazi cha taifa kinachoshughulikia janga la corona kitatoa taratibu siku ya Jumanne baada ya maelekezo ya rais, alieleza mmoja wa wanakikosi hao.

Museveni ameamuru pia kufungwa kwa maduka makubwa, njia tao, maduka ya vifaa, biashara zisizo za chakula, saluni, nyumba za kulala wageni na karakana za magari kwa siku 14, maeneo amayo amesema hukusanya watu wengi, limeeleza gazeti la Daily Monitor la Uganda.

Amri hiyo haihusu hospitali, maeneo yanayotoa huduma za kitabibu na mashirika yanayojihusisha na masuala ya afya.

Taarifa zaidi kuhusu coronavirus:

Rais amesema kuwa wakati serikali awali ikiweka marufuku ya watu kukusanyika, bado kumekuwa na mianya ya kusambaa kwa virusi.

Ingawa, alieleza kuwa kati ya watu 33 waliothibitishwa kuwa na maambukizi, watatu pekee walikuwa wasafiri waliopata maambukizi wakiwa safarini nje ya Uganda.

Wasafiri wengi hawakuheshimu hatua za kukaa karantini huku wengine walitoroka, na hakuna anayefahamu ni watu wangapi huenda wameambukizwa, na hii ndio sababu hasa ya kuweka hatua hizi mpya.

Museveni amesema maeneo muhimu kama ofisi za makampuni ya simu, benki, makampuni binafsi ya ulinzi yataendelea kuwa wazi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *