Cryptoqueen: Jinsi mwanamke huyu alivyoutapeli ulimwengu kisha kupotea


The Missing Cryptoqueen

Ruja Ignatova alijiita Malkia wa sarafu ya kidigitali al maarufu Crptocurrency. Aliwaeleza watu kuwa amebuni sarafu ambayo itatoa ushindani kwa Bitcoin na kuwashawishi kuwekeza mabilioni ya fedha, kisha miaka miwili iliyopita akatoweka.

Jamie Barlett alitumia miezi kadhaa kuchunguza ni jinsi gani alivyoweza kuwashawishi watu kupitia matangazo ya kibiashara ya kuwekeza katika sarafu za kidigitali na kujaribu kung’amua ni wapi anakojificha

Mapema mwezi Juni mwaka 2016, mafanyabiashara huyo mwenye miaka 36 aliyejiita Dkt. Ruja alisimama jukwaani katika ukumbi wa Wembley mbele ya maelfu ya mashabiki wake.

Kama ilivyokuwa kawaida yake, alikuwa amevalia gauni lenye bei ya tahamni la kuhudhuria hafla za jioni, hereni za ndefu za dhahabu na rangi nyekundu mdomoni.

Aliuleza umati huo kuwa sarafu yake ijulikanayo kama OneCoin inapigiwa upatu kuwa sarafu kubwa zaidi duniani ya kidijitali ambayo alidia kila mtu ataweza kufanya malipo kokote kule.

Bitcoin ndiyo ilikuwa sarafu ya kwanza ya kidjitali na bado inaslaia kuwa inayotambulika zaidi.

Kupanda kwa thamani yake kutoka mapeni kidogo hadi mamia ya dola kwa kila sarafu ilipofika katiakti ya mwaka 2016, imesababisha msisimko mkubwa miongoni mwa wawekezaji.

Watu wengi walitafuta kujihusisha na fursa hii mpya na ya kipekee.

Haki miliki ya picha
Shutterstock

Dr Ruja aliuambia umati katika ukumbi wa Wembley kuwa OneCoin ndiyo itakayoiangamiza Bitcoin akisema katika kipindi cha miaka miwili ijayo, hakuna atakayekuwa akizungumzia tena Bitcoin.

Kote ulimwenguni, watu tayari waliwakuwa wanawekeza kattika OneCoin, wakitumai kuwa sehemu ya mageuzi makubwa katika ulimwengu wa fedha za kidijitali.

Nyaraka zilizovujishwa kwa BBC zinaonesha Waingereza walitumia kima cha pauni milioni 30 kuwekeza katika OneCoin katika kipindi cha miezi sita ya kwanza za mwaka 2016, Pauni milioni mbili katika kipindi cha wiki moja pekee na kiwango cha uwekezaji kingeongezeka baada ya maonesho ya Wembley.

Kati ya Agosti 2014 na Machi 2017, zaidi ya Pauni bilioni 4 ziliwekezwa katika mataifa kadhaa. Kuanzia Pakistan, Brazil, Hong Kong, Norway, Canada, Yemen hadi Palestina.

Lakini kulikuwa na jambo moja muhimu ambalo hawa wawekezaji .

Kulieleza hilo, kwanza inabidi nitoe ufafanuzi jinsi sarafu ya kidijitali inavyofanya kazi.

Hii si rahisi, tembelea mitandao na utakuta maelezo karibu mia , mengine ya kushangaza hadi hata wasio na utaalamu kuhusu sarafu hii.

Ila la msingi kwanza kujua ni kwamba pesa zina thamani kwa sababu watu wengine wanadhani zina tahamni, Iwe ni noti au mapeni ya Benki ya Uingereza, mawe ya thamani au hata viberiti ambavyo vyote vilitumika kama fedha katika kipindi cha nyuma, hufanya kazi wakati ambapo kila mmoja anaamini.

Kwa muda mrefu, watu wamejaribu kutengeza sarafu za kidijitali ambazo ni huru dhidi ya sarafu zinazotumika na serikali, lakini wamekuwa wakishindwa kwasasabu watu hawaziamini sarafu hizo. Huwa wanahitaji mtu wa kutwishwa dhamana ambaye anaweza kudhibiti mgao wa sarafu hiyo na udanganyifu ni rahisi kufanyika.

Sababau ya kwanini watu wengi wanavutiwa na Bitcoin ni kuwa inasuluhisha matatizo hayo.

Inategemea mfumo maalumu wa kuweka data za watumiaji wake ujulikanao blockchain, ambo ni kama kitabu kikubwa ambacho wamiliki wa Bitcoin wana nakala zake,

Wakati wowote Bitcoin inatumwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, rekodi ya malipo hayo yananakiliwa kwa kitabu cha kila mmoja. Hakuna mtu, benki, serikali au hata walioanzisha sarafu hiyo anasimamia au anaweza kubadilisha mfumo huo wa kufanya biashara ya fedha.

Kuna mahesabu yanayohitaji werevu wa hali ya juu yanayotumika katika bishara hiyo ya Bitcoin ambayo inamaanisha kuwa hakuwezi kutengezwa sarafu ghushi, mfumo huo hauwezi kudukuliwa au kedha hizo za kidijitali kutumika mara mbili.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *