Darzeni ya wanafunzi wa madrasa watekwa nyara jimbo la NigerSerikali ya Niger imeandika kwenye ujumbe wake wa Twitter kwamba karibu wanafunzi 200 walikuwa katika shule hiyo ya Kiislamu wakati shambulio lilipotokea.

Taarifa zaidi zimesema haifahamiki bado ni wanafunzi wangapi waliotekwa nyara.

Utekaji huo umefanyika baada ya wanafunzi 14 kutoka chuo kikuu kimoja kaskazini magharibi mwa Nigeria wakishikiliwa kwa siku 40 kuachiliwa huru.

Katika habari nyingine msemaji wa polisi wa jimbo la Niger amesema kwenye taarifa watu waliokuwa na bunduki wakiwa kwenye pikipiki walishambulia mji wa Tegina katika wilaya ya Rafi jimbo hilo hilo jana saa tisa za mchana.

Hata hivyo hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusiana na shambulizi hilo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *