EAC : Rwanda, Uganda watafikia suluhu kabla ya mkutano wa AgostiLakini vyanzo vya habari katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) vinasema kuwa mvutano huu kati ya Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Uganda Yoweri Museveni unaonyesha kuwa kuna matumaini ya kufikia suluhu.

“…Kuna juhudi za ngazi ya juu kutafuta suluhu ya mgogoro huu. Rais wa Tanzania na Kenya na viongozi wengine katika eneo wanaendelea kuzungumza na viongozi hao wawili… Suala la mgogoro wa Uganda na Rwanda haliwezi kusubiri mkutano rasmi wa viongozi. Litashughulikiwa mapema,” afisa wa ngazi ya juu wa EAC amesema.

“Nimeanza kuhisi matamko ya Kagame yanaelekea kwenye kutafuta suluhu, na siyo kushambulia kama ilivyokuwa awali,” afisa huyo amesema.

Mkutano unaofuatia wa viongozi wa EAC umepangwa kufanyika Agosti, 2019, kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa sekretarieti ya EAC, lakini “iwapo kuna kitu cha haraka na muhimu, marais wa nchi hizo wanaweza kuitisha mkutano wakati wowote.”

Nje ya utaratibu wa mikutano ya EAC, viongozi hao wawili inawezekana wakakutana katika mikutano ya eneo na ya kimataifa ambayo wanaweza kuwa wanahudhuria.

Kwa upande mmoja, Kigali imeendelea kueleza kero lake kwa dunia, wakati Kampala imekuwa kwa namna fulani haionyeshi kuchukua hatua yeyote katika kukabiliana na suala hilo, gazeti la Daily Monitor la Uganda limeripoti Jumapili.

Hata viongozi wa Uganda, ambao mwanzoni mwa mgogoro huu walionyesha utashi wao wa kuzungumza na wenzao wa upande wa Rwanda juu ya kujibu madai yaliyotolewa dhidi ya Uganda, tangu wakati huo wamejizuia kufanya hivyo, vyanzo vya habari vimeeleza.

Kuanzia Februari 27, Rwanda ilifunga mipaka yake kwa kuzuia bidhaa za Uganda kuingia nchini humo, na tangia wakati huo imewakataza raia wake kusafiri kwenda Uganda, ikidai kuwa wananchi wake wanakamatwa kinyume cha sheria na kuteswa nchini Uganda.

Mwezi mmoja baada ya tukio hilo, hakuna mkutano wowote uliokuwa umetayarishwa katika ngazi yeyote uliotangazwa, na vyanzo vya habari vinasema hakuna mkutano kama huo uliokuwa umepangwa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *