Ethiopia: Mageuzi ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed yaibua upya uhasama wa kikabila


Abiy Ahmed

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Abiy Ahmed amebadilisha Ethiopia – lakini mzozo wa kijamii bado ni kizingiti kikubwa

Baada ya kuzindua mageuzi makubwa katika historia ya Ethiopia Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Dr. Abiy Ahmed, anakabiliwa na vitisho.

Mauaji ya mkuu wake wa jeshi na madai ya majaribio ya mapinduzi katika Jimbo la Amhara ni baadhi ya vitu vitakavyorudisha nyuma mchakato wa mageuzi hayo.

BBC inaangazia changamoto zinazomkabili kiongozi huyo mwenye umri mdogo katika bara la Afrika.

Wiki chache zilizopita, Abiy Ahmed alipongezwa kote Afrika kama kiongozi mwenye maono na anaependa mageuzi.

Aliwaachilia huru wafungwa wakisia , kuwateua wanawake zaidi katika baraza lake la mawziri, kuwashawishi wapinzani kuongoza bodi ya uchaguzi nchini na pia kuongoza mchakato wa kuafikiana na taifa jirani la Eritrea ambalo limekuwa likizozana na Ethiopia kwa miongo kadhaa.

Mwezi Disemba mwaka jana alipokutana na mwandishi wa BBC Fergal Keane, Dr. Abiy Ahmed alisema ulimwengu unatakiwa ukiangazia Ethiopia “ioneshe jinsi watu wanavyoweza kuishi pamoja kwa amani.”

Mamiliaoni wanakabiliwa na hatari

Baada ya jaribio la mapinduzi dhidi ya utawala wa Jimbo la Amhara ambapo mkuu wa majeshi aliyekuwa mshirika wake wa karibu,Jenerali Seare Mekonnen, kuuawa nafasi ya Bw. Abiy na hatma ya mageuzi yake huenda yakakabiliwa ni vikwazo.

Aliyedaiwa kupanga mapinduzi hayo alipigwa risasi na kuawa kufuatia msako mkali na kamata kamata ya washukiwa.

Lakini hakuna mtu anayeifahamu vizuri Ethiopia anaamini suala hilo limefikia kikomo.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Mkuu wa eneo la Amhara aliuawa pamoja na maafisa wengine wawili

Huku karibu watu milioni 2.5 wakiwa wametoroka makwao kutokana na ghasia za kikabila na mpasuko wa katika muungano wa wacham tawala cha EPRDF, Bw. Abiy anakabiliwa na kibarua cha ziada.

Sasa amegeuka kuwa mhasiriwa wa magauzi anayopigania kuleta nchini mwake.

Hiki ni kipindi kigumu kwa Ethiopia na waziri mkuu Abiy, ambaye anakabiliwa na mizozo ya ndani ya nchi.

Tangu uchaguzi wa mwaka jana, Abiy amekua akipambana kumaliza mvutano wa kisiasa kwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kuondoa makatazo dhidi ya vyama vya kisiasa na kuwashtaki maafisa wanaoshutumiwa kukiuka haki za binaadamu.

Makabila makubwa Ethiopia:

 • Oromo – 34.4%
 • Amhara – 27%
 • Somali – 6.2%
 • Tigray – 6.1%
 • Others – 26.3%

Chanzo: Makadirio ya CIA World Factbook, 2007

Ethiopia imegawanywa katika majimbo 9 ya kijamii ambayo yanajitawala.

Chini ya utawala wa Dergue suala la umoja wa kitaifa lilisisitizwa kwa nguvu zote katika miongo miwili ya utawala wa EPRDF uliofuatia.

Kupanuliwa kwa nafasi ya kisiasa chini ya utawala wa Bw. Abiykumezua upya taharuki za kijamii.

Mfumo wa utawala wa wa kijamii nchini Ethiopia umekuwa ukigubika siasa za taifa hilo kwa muda mrefu.

Na kasi ya mageuzi ya Bw. Abiy haijapokelewa vyema na vyama vinne vinavyoshirikiana na chama tawala.

Kutengwa kwa jamii ya Tigray iliyo na 6% ya watu wote nchini humo na ambao walikuwa na nafasi kubwa katika utawala uliopita kunaendelea kupandisha joto la kisiasa.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Mamilioni ya watu wamefurushwa makwao kufuatia mapigano ya kikabila

Tunataka kuojiondoa

Katika Jimbo la Oromia na Amhara – ambayo yana idadi kubwa ya watu- vyama vidogo vinavyopigania maslahi y akijamii vimeibuka.

Mtu anayeshukiwa kupanga mapinduzi ya Amhara yaliyotibuka analaumiwa pia kwa kuwasajili vijana kuwa wanamgambo wa kijamii.

BBC ilitembelea kambi ya wakimbizi iliyo na watu takribani 700,000 ambako watu wa jamii ya kisomali wamekuwa wakizozana na majirani zao Waoromo.

Mmoja wa wanawake wazee waliotembea kwa majuma kadhaa kufika katika kambi hiyo ya wakimbizi alisema:

“Tulikuwa tukiishi kwa amani lakini Waoromo wanaoishi katika eneo hilo walisema: ‘Idadi yenu inazidi kuongezeka ikilinganishwa na Waethiopia wengine kwa hiyo tunataka muondoke’. Baada ya hapo mapigano yalizuka ambapo wanaume walichinjwa na watoto kuauawa, Hiyo ndio sababu tulikuja hapa kutafuta amani.”

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Nchini Ethiopia imetawaliwa na ghasia za maandamano ya kabila la Oromo ambalo limekuwa likifanya maandamano ya kuipinga serikali tangu mwaka 2015

Chuki za kikabila hazimaliziki chini ya utawala wa kidikteta bali zinajificha lakini huibuka tena serikali kama hii ya Waziri mkuu Dr. Abiy inapojaribu kuleta mageuzi.

Dr. Abiy sasa anastahili kuwa makini zaidi anapoendeleza agenda yake ya mageuzi.

Kamata kamata inayoendelea baada ya jaribio la mapinduzi Amhara ambapo zaidi ya watu 250 wanazuiliwa – huenda ikazidisha chuki katika jimbo hilo.

Kuzimwa kwa huduma za intaneti katika wiki za hivi karibuni huenda kulilenga kulemza juhudi za mahasimu wake lakini hali ilivyo kwasasa taifa limegubikwa na taarifa za uvumi kuhusu sababu kamili ya kukatiza huduma hiyo muhimu ya mawasiliano.


Abiy Ahmed ni nani?

Haki miliki ya picha
Getty Images

 • Abiy alizaliwa Agaro kusini Ethiopia katika eneo la Jima tarehe 15 Agosti 1976 na baba Mwislamu kutoka jamii ya Oromo na mama Mkristo kutoka jamii ya Amhara.
 • Dkt Abiy anaangaliwa kama mwanasiasa mwenye kukubalika ambaye ana siasa ya kuwashirikisha watu katika masuala yanayowahusu, na mwenye mafanikio makubwa upande wa elimu na jeshi.
 • Ana taaluma ya udaktari katika masuala ya amani na usalama kutoka chuo kikuu cha Addis Ababa na ana shahada ya uzamili ya mabadiliko ya uongozi kutoka Chuo Kikuu cha Greenwich, London Uingereza.
 • Ana shahada ya uzamifu katika usimamizi (MBA) chuo kikuu cha Ashland Leadstar aliyoipata 2013 baada ya kukamilisha masomo yake ya shahada ya kwanza ya Kompyuta kutoka chuo cha habari cha Microlin mjini Addis Ababa mwaka 2001.
 • Abiy anazungumza vizuri lugha za Afan Oromo, Amharic na Tigrinya, pamoja na Kiingereza.
 • Akiwa kijana mdogo miaka ya 1990, alijiunga na mapambano ya kijeshi dhidi ya utawala wa zamani wa Dergue.
 • Baada ya kuanguka kwa utawala wa Dergue, alipata mafunzo rasmi ya kijeshi katika chuo cha Brigade Asefa Magharibi mwa Welega na akapanda cheo haraka na kuwa Luteni kanali na baadaye alihudumu kwa kiasi kikubwa katika huduma za ujasusi na mawasiliano.
 • Mnamo mwaka 1995, alihudumu katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Rwanda.
 • Wakati wa mzozo wa mpaka baina ya nchi yake na Eritrea kati ya mwaka 1998 hadi 2000, aliongoza kikosi cha ujasusi kilichokuwa na jukumu la uchunguzi katika eneo lililochukuliwa na vikosi vya jeshi la Eritrea.
 • Mwaka 2007, alianzisha shirika la Ethiopia la Mtandao wa Taarifa za Usalama (INSA) ambapo alihudumu kama mjumbe wa bodi ya Mawasiliano ya simu ya Ethiopia, Ethiopia Televisheni na mashirika mengine ya serikali.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *