Fahamu kuhusu ugonjwa ambapo ngozi hujibambua yenyewe


Anna's leg with eczema

Anna Byard-Golds amekuwa na ugonjwa wa kubambuka ngozi katika maisha yake yote.

“Nilianza kujitambua nikiwa na umri wa miaka minne au mitano. Niligundua kuwa mikono yangu ni tofauti na ya watoto wengine na pia nilihisi sifanani na wengine,” amezungumza na kipindi cha BBC cha Newsbeat.

Inaseekana kuwa asilimia 89 ya watu wazima wenye ugonjwa wa ngozi kujibambua wanahisi kuwa umuhimu wao ni kidogo sana maishani.

Robo ya watoto wenye ugonjwa huu wa ngozi wanajidunisha, kwa mujibu wa wazazi walioshiriki utafiti.

“Ni kama ngozi ya kifaru- ina mabaka na mipasuko, ni ngumu na isiovutia,” Anna, 15, anasema.

Anna amerejea shule lakini kuna siku nyingi tu anazokumbuka ambazo huwa hataki kwenda shuleni.

“Kuna siku ambazo ningekuja nyumbani mapema kwasababu ngozi yangu inauma kweli.

“Inakuwa vigumu kusogea, kuandika huwezi, kwahiyo sikuweza kufuatilia masomo kama inavyotakikana.”

Nyakati za asubuhi, ugonjwa wake wa kujibambua ngozi ungeenea hata kwenye uso na kumfanya kukosa kujiamini.

“Kuna siku ambazo ngozi inajibambua kweli. Ninachotaka wakati huo ni kuitoa kabisa ngozi yangu.”

“Sikutaka watu wanione. Nilihisi aibu.”

Maelezo ya picha,

Ngozi ya Anna ambayo hubambuka yenyewe

Akiwa anakua, Anna alionewa na watoto wenzake kwasababu ya ugonjwa wake wa ngozi.

“Sikujua tu kuwa mimi ni tofauti, lakini pia watu wengine waliniambia kuwa siko kama wao.”

Anna alivaa nguo kubwa kubwa kujaribu kufunika ngozi yake kwasababu hakutaka yeyote ajue ana ugonjwa wa ngozi kujibambua.

“Na hilo liliniathiri kwasababu unahisi hauko kama wengine.

Moja ya changamoto zilizobainiwa na watafiti ni kujitenga.

Hali haikuwa tofauti kwa Anna – angeonana na rafiki zake lakini kama yuko ndani tu.

“Kila wakati nilikutana na rafiki zangu ama kwetu au kwao lakini sio maeneo ya nje kwasababu niliona haya.

“Wakati mwingine unahisi wewe ni mzigo.” Kwa wengine.

Maelezo ya picha,

“Nilipokuwa mimi bila kufikiria kile ninachopitia”

Mbinu alizotumia Anna kukabiliana na hali yake ni pamoja na kujipaka dawa, kusikiliza muziki na kutazama video akiwa ndani ya nyumba.

“Nikiwa peke yangu, nilihisi ninahukumiwa juu ya ngozi yangu lakini nikiwa nafanya kazi zangu nilijihisi kuwa mtu tofauti.”

“Sehemu moja ya kukabiliana na hali hii ni kujiamini na kuwa na fikra chanya”, Anna anasema.

“Imenichukua muda kujua kwamba unahitaji kuwa na mtazamo chanya la sivyo huwezi kufikia unacholenga,” Anna ameongeza.

Pia anasema ni muhimu kuacha hisia kuchukua mkondo wake.

“Kama unataka kulia, lia haswa mpaka utosheke, na pia unahitaji kuzungumza na watu wako wa karibu ili waelewe unavyohisi.

“Kuna siku unajiuliza, ‘Kwanini mimi nipitie haya na wala sio mwingine?’ Wakati kama huo nilijipata nikibubujikwa na machozi.”

Kuna dawa ambayo Anna ameanza kuituia na sasa hali yake inaendelea kuimarika.

Lakini licha ya kwamba mikono yake haionekani tena kuwa na rangi nyekundu na kufura, haimaanishi kwamba amepata tiba.

Kulingana na mtaalamu wa ngozi Julie Van Onseleme, “sio suala la kutibu ugonjwa wa kubambuka kwa ngozi bali namna ya kujua kuudhibti”.

Julie anaongeza: “Hata ukipata tiba itakayokupa afueni, bado ugonjwa huo utakuwa nao na unachohitajika kujua ni namna ya kutunza ngozi yako”.

Kwa Anna, bado ngozi yake hupasuka, inafura pamoja na kubadilika rangi hasa kwenye uso na viganja vya mkono.”

Lakini sasa hivi amepata afueni.

“Sasa naweza kujiangalia kwenye kioo bila kufikiria vinginevyo kama vile: Sitaki kukuona.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *