Félicien Kabuga: Mahakama ya Ufaransa yaamuru mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda ashtakiwe Tanzania


Félicien Kabuga

Maelezo ya picha,

Félicien Kabuga, wakati mmoja alikuwahi kuwa mtu tajiri zaii nchini Rwanda na alitumia majina 28 bandia kukwepa kukamatwa

Mahakama moja ya kukata rufaa nchini Ufaransa imekubali kumpeleka msukiwa a mauaji ya kimbari nchini Rwanda Felicein kabuga kushatkiwa nchini Tanzania. Bwana kabuga alikamatawa nyumbani kwak nje ya mji wa Paris baada ya miaka 26 kama mtoro.

Takriban watu 800,000 waliauwa nchini Rwanda katika mauaji ya kimbari ya 1994. Bwana kabuga anadadaiwa kupitisha fedh a katia makundi ya waasi akiwa mwenyekiti wa kitaifa wa hazina ya ulinzi ya kitaifa.

Ammekana madai yote hayo. Wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake mwezi Mei, alielezea madai hayo kama ya uwongo.

Je Filicien Kabuga ni nani?

Ndiye aliyekuwa mtu tajiri zaidi nchini Rwanda kabla ya mauaji ya 1994.

Akijipatia utajiri wake kupita bishara ya majani ya chai mwaka 1970 na alifanya biashara katika sekta chungu nzima nyumbani na katika mataifa ya kigeni.

Alikuwa mshirika wa karibu wa chama tawala cha MRND – na alikuwa na uhusiano na rais wa zamani Juvenal Habyarimana ambaye alifariki 1994.

Akituhumiwa kwa kuwa mfadhili mkuu wa mauaji hayo na kutumia biashara yake na uwezo wake kupanga na kufadhili mauaji.

Mmiliki wa kituo cha redio ya kibinafsi RTLM alishutumiwa kwa kuwachochea watu wa kabila la Hutu kuwaua Watutsi.

Mwaka 2006, jopo la kimataifa la Rwanda lililokuwa likichunguza mauaji hayo lilisema lina ushahidi kwamba bwana Kabuga alizuru nchini Kenya ama hata kuishi nchini humo, ambapo alikuwa akisimamia maslahi yake ya kibishara.

Miaka mitatu baadaye, Bwana Stephen Rapp, ambaye alikuwa balozi wa Marekani aliishutumu serikali ya Kenya kwa kukataa kumtoa bwana Kabuga.

Kulikuwa na ushahidi kwamba bwana Kabuga alihudhuria hafla zilizoshirikisha watu maarufu, alisema madai ambayo Kenya imekana.

Ni wazi kwamba familia ya bwana Kabuga ilikuwa ikimiliki mali nchini Kenya baada ya mali moja kuzongwa na kesi 2015 wakati mkewe, Josephine Mukazitoni , ambaye alikuwa mmiliki mwenza , alipojaribu kumiliki.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *